· Julai, 2013

Habari kuhusu Mahusiano ya Kimataifa kutoka Julai, 2013

Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu

Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama kinachoongoza maandamano kinasema kwamba utawala uliopo hauna dhamira ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na kwamba serikali imeng'ang'ania madarakani. Kiongozi wa...

Je, Ziara ya Obama Barani Afrika ni Neema au Hasara?

Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya siku sita katika nchi tatu za Kiafrika, Senegali, Afrika Kusini na Tanzania, mnamo Julai 2, 2013. Obama alitangaza mradi mpya, "Umeme Afrika", kukuza matumizi ya umeme mara dufu katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Maoni ya watu duniani kote juu ya umuhimu na matokeo ya ziara hiyo yamegawanyika mno.

Obama Barani Afrika: Vita ya Kibiashara na China?

Rais Obama ametembelea bara la Afrika kwa ziara iliyokuwa imepangwa kati ya tarehe 26 mpaka Julai 3, 2013. Hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini baada ya kutembelea Senegali na baadae aliitembelea Tanzania. Wachambuzi wengi wanaoiona safari hiyo kama mpango wa kushindana , kama jaribio la Marekani kupambana na mafanikio ya kiuchumi ya China katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.