· Julai, 2013

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Julai, 2013

Barua ya Wazi ya Kushinikiza Kuachiwa Huru kwa Mwanasheria

  24 Julai 2013

Mnamo Julai 23, 2013, zaidi ya raia 400 wa China wamesaini barua ya kushinikiza serikali ya China kumuachia huru Xu Zhiyong, ambaye ni mwanasheria mashuhuri na mpigania haki aliyekamatwa mnamo Julai 16 baada ya kushinikiza kuachiwa kwa wanaharakati pamoja na kuratibu kampeni dhidi ya uovu unaofanywa na serikali. MRADI WA...

India: Chakula Chenye Sumu Chaua Watoto 24

  18 Julai 2013

Chakula kilichoua wanafunnzi na kuwaacha wengine katika hali mbaya kinasadikiwa kuwa kilichanganyikana na dawa ya kuulia wadudu. Tukio hili linaibua maswali kuhusiana na ubora wa chakula cha mchana wanachopewa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini.

Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

  6 Julai 2013

Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.