· Mei, 2013

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Mei, 2013

Botswana: Kuibwa kwa Kazi ya Sanaa ya “Bushman's Secrets”

MyWeku anaichambua filamu yenye maudhui halisi (documentary) inayoelezea wizi wa kazi ya sanaa ya Sana iitwayo “Bushman's secrets”: Filamu hii inachora picha inayosikitisha ya namna ambavyo Uniliver, kampuni inayojinadi kama “mzalishaji mkubwa tena nambari moja duniani wa barafu zitengenezwazo kwa maziwa maarufu kama ice cream,” sasa linatumia bila aibu maudhui...

Rais wa Chama cha Madaktari Msumbiji Akamatwa

Baada ya mgomo wa madaktari uliodumu kwa takribani juma moja nchini Msumbuji, Dr. Jorge Arroz, Rais wa Associação Médica de Moçambique, amekamatwa usiku wa Jumapili, Mei 26, 2013, kwa tuhuma za “uchochezi” (kuhamasisha watu kutokuridhishwa au kuiasi serikali). Kwenye mtandao wa Twita na Facebook, @verdademz, @canal_moz na ripoti nyingine za...

Maelfu ya Wafanyakazi Waandamana Barani Asia

  4 Mei 2013

Global Voices inayapitia kwa haraka maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kwenye nchi za Cambodia, Filipino, Indonesia na Singapore. Mikutano, ambayo iliandaliwa kudai haki za wafanyakazi na makundi mengine ya utetezi, yalifanyika kwa amani katika bara lote la Asia ya Kusini Mshariki.

Ethiopia: Mwanablogu Ahukumiwa Miaka 18 Jela kwa “Kuvunja Katiba”

GV Utetezi  4 Mei 2013

Mnamo Mei 1, Mahakama Kuu ya Ethiopia ilitoa hukumu kali kwa mwandishi aliyeshinda tuzo Eskinder Nega, ambaye sasa atatumikia kifungo cha miaka 18 jela. Mohamed Keita wa Kamati ya Kuwalinda Waandishi anasema, “Kushitakiwa na hatimaye kutiwa hatiani kwa Eskinder na waandishi wengine ni dalili za utawala unaoogopa maoni ya raia wake.”