· Disemba, 2012

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Disemba, 2012

Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.

Video ya Kuomba Ujenzi wa Vyoo vya Umma huko Jharkhand, India

  30 Disemba 2012

Amit Topno, mwakilishi wa jumuiya ya hiari “inayopiga picha za video” aliripoti kwamba wakati wa kijiji cha Nichitpur katika Jimbo la Jharkhand hawana choo chochote cha umma kinachotumika. Wanavijiji wanaziomba mamlaka za serikali za mitaa kupitia video hii kuhakikisha kuwa vyoo vinavyostahili matumizi ya binadamu vinajengwa.

Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan

  23 Disemba 2012

Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti...