· Juni, 2012

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Juni, 2012

Sudani: Kuondoa kizuizi cha Mapinduzi ya Sudani

Tofauti na nchi nyingine katika eneo lake, Sudani mara nyingi huwa haipati nafasi katika vyombo vikuu vya habari, na hili lilikuwa wazi zaidi wakati wa maandamano yalifanyika Ijumaa na Jumamosi. Sababu ni kwamba serikali ya Sudani imevibana mno vyombo vya ndani vya habari na kuwazuia waandishi kuripoti habari zinazohusu masuala ya haki za binadamu na ufisadi.

Ethiopia: Ardhi, Historia na Haki katika Eneo la Gambella

Wanaharakati wa masuala ya ardhi wanatumia hati ya malalamiko ya mtandao, mtandao wa facebook na twita kufanya kampeni dhidi ya unyang’anyi wa ardhi nchini Ethiopia. Inaarifiwa kwamba wanakijiji kwenye jimbo msikini zaidi nchini humo, Gambella, wanalazimishwa kuhamia kwenye vijiji vilivyobuniwa na serikali ili kuwapisha wanaoitwa 'wawekezaji' wakubwa.

Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi

  12 Juni 2012

Jarida la Ocas linalosambazwa katika mitaa ya mjini São Paulo pamoja na Rio de Janeiro tangu 2002, ni jarida ambalo husheheni habari ambazo hulitofautisha na vyombo vikuu vya habari nchini Brazil. Na linakwenda zaidi ya hapo. Aidha huwapa mwanzo mpya na fursa za kazi watu ambao hawana makazi na ambao wamo katika hatari ya kuangamia kijamii.