Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Agosti, 2010
Irani: Kampeni ya Kutaka Mwanablogu-Mpiga Picha Hamed Saber Kuachiwa Huru
Zaidi ya wanafunzi 70 waliohitimu elimu ya chuo kikuu na wasomi wa nchini Irani wametoa wito wa kuachiwa kwa Hamed Saber, ambaye ni mwanablogu-mpiga picha na mwanasayansi wa kompyuta wa nchini humo aliyekamatwa pasipo sababu za kuelewekea mnamo tarehe 21 Juni 2010 jijini Tehran.
Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam
Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.