· Januari, 2010

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Januari, 2010

Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa

Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.

Misri: wanablogu Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutembelea kwao Naha Hammady

Leo Misri iliwatia mbaroni wanablogu 20 waliokuwa wakitembelea eneo la Naga Hammady huko Misri ya Juu ili kutoa heshima zao kwa watu waliouwawa katika shambulio la kidini mnano January 7 mwaka huu. Watu 7 waliuwawa kwa risasi huku wengine wengi wakijeruhiwa pale mwuaji alipowamiminia risasi Wakristo wa Madhehebu ya Kikopti waliokuwa wakitoka kanisani mara baada ya Misa ya Krismas (Wakopti husherehekea Krismas kila tarehe 7 Januari). Uamuzi wa kutembelea eneo hilo uliofanywa na wanablogu hao ulikuwa ni kwa lengo la kuungana dhidi ya uhasama wa kidini.

China: Kwa Heri Google

  13 Januari 2010

Kufuatia tangazo la Google leo kuwa ikiwa serikali ya China haitaruhusu tawi lake la China kusitisha uzuiaji wa matokeo ya kutafuta tawi la Google nchini China litafungwa, wanamtandao walitembea mpaka kwenye ofisi za Google mjini Beijing ili kuweka maua. HABARI MPYA: picha zaidi hapa, uwekaji rasmi wa maua (ya rambirambi)...

China: Adhabu ya Kifo kwa Akmal, ni Tendo la Kufuta Aibu ya Zamani

  2 Januari 2010

Akmal Shaikh, raia wa Uingereza aliyeshtakiwa kwa kuingiza mihadarati kinyume cha sheria nchini China, aliuwawa siku ya Jumanne japokuwa familia yake pamoja na serikali ya Uingereza waliomba adhabu ipunguzwe, wakidai kuwa alikuwa ni mgonjwa wa akili. Mahakama Kuu ya China hata hivyo ilikataa ombi la kuangalia hali ya akili ya...