· Disemba, 2009

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Disemba, 2009

Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”

  23 Disemba 2009

Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.

Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani

  20 Disemba 2009

Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.

Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani

Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.

Indonesia: Sarafu za Kudai Haki

  8 Disemba 2009

Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.

Guatemala: Kuvunja Milango ya Madanguro

  6 Disemba 2009

Blogu inayojulikana kama Noticias para Dios inatoa habari za ndani, kama vile mambo yenyewe yanavyotokea pasipo kuficha kitu, kuhusu maisha ya kila siku ya mwanasheria wa Ki-Guatemala anayejaribu kuwaokoa watoto kutoka kwenye madanguro ambako wamekuwa wakiishi baada ya kuchukuliwa kutoka makwao.