· Januari, 2010

Habari kuhusu Historia kutoka Januari, 2010

Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa

Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.

China na Hong Kong: Walinzi na Wauaji

  5 Januari 2010

Bodyguards and Assassins (Walinzi na Wauaji) ni filamu ya kuchangamsha iliyotolewa wakati wa Krismasi huko China, Hong Kong na Taiwan. Ikiwa ni filamu ya kizalendo, awali ilipangwa kutolewa mwezi Oktoba ili kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Watu wa China lakini ikacheleshwa mpaka mwisho wa mwaka 2009. Tofauti...