The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Governance Hifadhi ya mada

Kiungo cha RSS kwa Governance

2009-10-26

Japan: Uchunguzi Mpya Juu ya Umaskini Waharibu Soga za Utajiri

Mjapani mmoja kati ya sita anaishi katika umasikini inasema ripoti mpya ya Wizara ya Ustawi wa Jamii [en]. Kwa mujibu wa takwimu za OECD, Japan ina kiwango kikubwa zaidi cha umasikini katika dunia iliyoendelea na ni ya 4 baada tu ya Mexico, Uturuki na Marekani. Mnamo mwezi wa Septemba, Makoto Yuasa, ...

2009-10-25

South Asia

Tshering Tobgay, kiongozi wa chama cha upinzani katika Bunge la Taifa la Bhutan, anatoa maoni kuwa: “mpito wetu kuelekea demokrasi, kwa hakika, umetukia bila mikwaruzo. Umetukia bila mikwaruzo kiasi kwamba wengi wetu walikuwa hata hawaufuatilii.”

Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

Juma lililopita huko Hammond, Louisiana, wapenzi wawili walituma maombi ya kibali cha kufunga ndoa na walikataliwa kwa misingi ya rangi zao tofauti. Afisa wa kutathmini na kuandikisha nyaraka (Muamuzi wa Amani) alidai kuwa “ndoa baina ya watu wa rangi hazidumu” na alisema kuwa anafanya hivyo “kwa ajili ya watoto.”

2009-10-24

Americas

“Kila siku ambayo ninapitia habari ninazidi kushawishika kuwa ninataka kuachana na klabu ya ‘Mimi ni Mtrini’ na kwenda sehemu nyingine”: Coffeewallah ameshachoka na kila kitu kuanzia uhalifu mpaka kodi.

2009-10-19

Sub-Saharan Africa

Kampeni ya kukomesha Chanjo kwa kulazimishwa nchini Namibia imezinduliwa: “ umoja wa Asasi za kijamii umetoa wito kwa Wanamibia wote kujiunga na kampeni ya kulaani chanjo kwa wanawake waishio na VVU bila ya ridhaa yao.

2009-09-26

Marekani: Stempu ya Iddi Yachochea Chuki Huko Tennessee

Barua pepe yenye madai ya uongo kuwa Rais Obama ametoa stempu mpya kuadhimisha sikukuu ya Waislamu Eid al-Fitr imemfikia Meya wa Tennessee ambaye aliisambaza kwa wafanyakazi wake na waasa waisusie stempu hiyo.

2009-08-31

Pakistani: Tatizo La Sukari Limeifanya Ramadhani Kuwa Chungu

Upungufu wa sukari pamoja na kupanda kwa bei nchini Pakistani mwaka huu kumewaathiri walaji na kumesitisha ongezeko la matumizi wakati wa mwezi wa ramadhani. Wanablogu wa kipakistani wanaichambua hali hiyo.

2009-08-18

China: Mitizamo Potofu Pamoja na Ubaguzi wa Wa-Han Dhidi ya Wa-Uyghur

Ni mwezi mmoja na zaidi umepita tangu machafuko ya Xinjiang ya Julai 5 na wengi wa wanamtandao wa intaneti wa Kichina bado wanazilaumu nchi za Magharibi pamoja na Rebiya Kadeer kwa kuwatetea wale wanaotaka kujitenga huko Xinjiang. Hata hivyo, kuna sauti za minong’ono zinazochepuka hapa na pale katika intaneti ya ...

2009-08-16

Palestina: Maoni Juu ya Kuzinduliwa Kwa Huduma ya Google.ps

Google imeongeza anwani ya google.ps (google palestina) kwenye orodha yake zana inayotoa huduma za utafutaji zinazolenga sehemu mbali mbali. Anwani hiyo mpya inakusudiwa kufanya kazi katika ukanda wea Magharibi na Gaza, ambako watoaji huduma za intaneti hufanyia kazi zao.

2009-07-27

Mauritania: Uchaguzi wenye udanganyifu?

Tarehe 18-07-2009, miezi 11 baada ya mapinduzi ya kijeshi yakiongozwa na Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz, Mauritania imemchagua Jenerali huyu kwa Urais, na kusababisha wapinzani wakuu wa Abdel Aziz kuukataa uchaguzi kwamba ni “kiini macho,” kwa mujibu wa Habari za BBC. Pitio la haraka haraka kwenye blogu za nchi za Saheli linaonyesha kwamba wapinzani wako katika ushirika mzuri.