· Januari, 2010

Habari kuhusu Utawala kutoka Januari, 2010

Rais wa Malawi kutangaza rasmi penzi lake siku ya Valentine

Wamalawi wanatafakari taarifa kuwa mnamo tarehe 1 Mei, rais wa nchi Dkt. Bingu wa Mutharika anatarajiwa kumuoa waziri wa zamani wa utalii Callister Moyo. Harusi hiyo itatanguliwa na sherehe za kitamaduni za uchumba wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino tarehe 14 Februari. Wanabloga wachache wamemtakia heri rais katika mapenzi mapya aliyoyapata baada ya kifo cha mkewe Ethel miaka mitatu iliyopita.

Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa

Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.

Misri: wanablogu Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutembelea kwao Naha Hammady

Leo Misri iliwatia mbaroni wanablogu 20 waliokuwa wakitembelea eneo la Naga Hammady huko Misri ya Juu ili kutoa heshima zao kwa watu waliouwawa katika shambulio la kidini mnano January 7 mwaka huu. Watu 7 waliuwawa kwa risasi huku wengine wengi wakijeruhiwa pale mwuaji alipowamiminia risasi Wakristo wa Madhehebu ya Kikopti waliokuwa wakitoka kanisani mara baada ya Misa ya Krismas (Wakopti husherehekea Krismas kila tarehe 7 Januari). Uamuzi wa kutembelea eneo hilo uliofanywa na wanablogu hao ulikuwa ni kwa lengo la kuungana dhidi ya uhasama wa kidini.

Thailand: “Tumechoshwa na Wizara ya Utamaduni”

  12 Januari 2010

Ukurasa wa wapenzi wa Facebook umezinduliwa na raia wa mtandaoni wanaokosa njia na sera za Wizara ya Utamaduni ya Thailand. Wizara hiyo imekuwa ikidhibiti sana uhamasishaji na usimamizi wa utamaduni wa asili wa Ki-Thai katika tovuti za vyombo vya habari vya kizamani na hata vile vya kisasa.