Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Mei, 2014
Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia
Ghasia, zilizofumuka baada ya kuuawa kwa kijana wa miaka 19, zilisababisha misuguano kati ya watu wenye asili ya Albania na Masedonia kwenye jiji la Skopje.
Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti
Kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji wa Kitibeti Gepe nchini China,hapa ni mtiririko wa matukio ya jinsi hiyo sambamba na video za nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube.
Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini
Ingawa Rwanda imepiga hatua kubwa katika kuponya majeraha ya mauaji ya kimbari ya 1994, makundi ya utetezi yanaripoti vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu.
Ethiopia: #FreeZone9Bloggers Yavuma Kwenye Mtandao wa Tumblr
Global Voices Advocacy ilianzisha mtandao wa Tumblr mapema mwezi Mei kutafuta uungwaji mkono kwa wanablogu tisa na waandishi wa habari – ambao wanne kati yao ni wanachama wa Global Voices – ambao kwa sasa wako kizuizini nchini Ethiopia shauri ya kazi zao. Washirika kutoka duniani kote waliwasilisha picha, ujumbe wa...
Mazungumzo ya GV: Kupigania Kuachiliwa Huru kwa Wanablogu wa Ethiopia wa Zone 9
Wanablogu tisa ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ---wanne wao wakiwa ni wanachama wa Global Voices ---wanashikiliwa nchini Ethiopia kwa sababu ya kutekeleza majukumu yao. Fahamu namna ya kuunga mkono kampeni ya #FreeZone9Bloggers!
‘Hali Mbaya’ ya Haki za Binadamu Nchini Vietnam
Mtandao wa haki za Binadamu illitoa ripoti yake ya 2013 kuhusu ‘hali mbaya’ ya haki za binadamu nchini Vietnam: …. Hali ya haki za binadamu nchini Vietnam iligeuka na kuwa mbaya mwaka 2013. Idadi ya watu waliotiwa kizuizini kwa kutoa maoni ya kisiasa yaliyo kinyume na wale wa chama tawala...
Kwa Nini Kublogu ni Tishio kwa Serikali ya Ethiopia
Beza Tesfaye anaelezea kwa nini kublogu ni tishio kwa serikali ya Ethiopia kufuatia kukamatwa kwa wanablogu tisa Ethiopia: Ninapoandika haya, Kwa uwoga nakumbushwa kwamba nchini Ethiopia, kutoa maoni yako kunaweza kukufanya uakapewa tiketi ya daraja la kwanza gerezani. Kutoka Aprili 25 hadi 26, 2014, wanablogu tisa wa Ethiopia na waandishi...
Ungana na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers Twita Mei 14
Ungana na wanablogu wa Global Voices kwa ajili ya kampeni ya kutwiti barani Afrika kwa ajili ya kuunga mkono wanablogu na waandishi wa habari tisa waliokamatwa mwishoni mwa mwezi Aprili na kwa sasa wako rumande nchini Ethiopia.
China Yamweka Kizuizini Mwanasheria wa Haki za Binadamu Pu Zhiqiang
Hii si mara ya kwanza kwa Pu Zhiqiang kuwekwa kizuizini. Akiwa mkosoaji maarufu wa sera za serikali ya China, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama wa nchi hiyo.
Sio Rahisi Ukiwa Mtu Mweusi Nchini Cuba
Habari mbaya kwa Wa-cuba wenye ngozi nyeusi au yenye mchanganyiko wa weusi na weupe ni kwamba hakuna taasisi huru za kisheria itawalinda kutelekezwa na serikali. Iván anaripoti kuwa watu wasio wazungu bado wanaendelea kubaguliwa nchini Cuba.