· Septemba, 2013

Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Septemba, 2013

Serikali ya Tanzania Yafunga Magazeti Mawili

  28 Septemba 2013

Serikali jana (terehe 27 Septemba, 2013) ilitangaza kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kuandika habari na makala zilizoelezwa zina nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola na kuhatarisha amani. Taarifa ya kufungiwa magazeti hayo ilisema; Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14)...

Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri

Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni. Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini...