· Julai, 2010

Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Julai, 2010

Lebanoni: Utawala wa Dinosauri

Punde baada ya matukio ya unyanyasaji ya hivi karibuni nchini Lebanon, Msemo wa “Utawala wa Dinosauri” ulianza kutumika na wanaharakati wa mtandaoni kwenye kampeni dhidi ya uvamizi wa namna hii katika mitandao yao. Mwanablogu wa Lebanon Tony anaeleza maana ya msemo huo.

Ivory Coast: Mwanablogu na Mwandishi wa Habari Théophile Kouamouo Akamatwa Pamoja na Timu Yake Tangu Julai 13

Waandishi wa habari watatu wa Le Nouveau Courrier d'Abidjan walitiwa mbaroni na polisi baada ya kukataa kueleza vyanzo vya habari vya uandishi wao wa kipelelezi kuhusu biashara ya usafirishaji kahawa na kakao kwenda nje ya nchi. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa raia na vyombo vya habari nchini Ivory Coast huku wenzao watatu wakiendelea kupigania kuachiwa kwa wanahabari hao.