Habari kuhusu Filamu

Filamu 14 za Mazingira zenye Kuvutia

  13 Novemba 2013

TVE (Televisheni inayohusika na Mazingira) yaonesha video 14 bora za washindani waliofika fainali kwenye shindano la kimataifa la filamu bora ya mazingira. Washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia wametengeneza filamu zinazochukua muda wa dakika 1 kwa kuzingatia mada zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo endelevu pamoja na bayoanuai....

Timu ya Soka ya Brazil Yazindua Kampeni Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi

  3 Novemba 2013

Katika video iliotolewa Jumatatu, Agosti 12, timu ya soka ya Grêmio of Porto Alegre ilileta pamoja baadhi ya wachezaji muhimu kwenye orodha ya majina yake, weupe na weusi, kwa majadiliano juu ya ubaguzi wa rangi. Mpango huo ulifanyika kusaidi mpango mpya wa FIFA, uliotekelezwa Mei mwaka huu na kupitishwa bila...

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

The Team Tanzania (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia: […] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika...

Ajentina: Dokumentari Kuhusu Wenyeji wa Mjini Yatafuta Tafsiri ya Maandishi

  30 Aprili 2012

Dokumentari iitwayo Runa Kuti iliyoshirikishwa katika mradi wa Haki miliki wa “Creative Commons” kuhusu kutambuliwa kwa wananchi waliotokana na uzao wa wenyeji wa zamani walioishi mjini katika jiji la Buenos Aires, inatafuta watu wa kujitolea kusaidia kuiwekea video hiyo tafsiri ya maandishi kwenda katika lugha za asili za Ajentina kama ki-Quechua, ki-Aymara, -kiMapuche na ki-Guaraní pamoja na ki-Kiingereza.

Dondoo za Video: Utetezi wa haki za binadamu

Kuna masimulizi kusisimua katika siku za hivi karibuni kwenye tovuti ya Global Voices Video za Utetezi ikiwa ni pamoja na haki za wananchi wenyeji na habari za hivi karibuni kutoka Amerika ya Kusini, Mashariki ya Mbali, Ulaya Magharibi na Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zilizochaguliwa na Juliana Rincón Parra.