· Mei, 2013

Habari kuhusu Mazingira kutoka Mei, 2013

China Yadhibiti Habari za Maandamano Yakupinga Kujenga Kiwanda cha Kemikali

  6 Mei 2013

Wakazi wa jiji la kusini magharibi mwa China liitwalo Kunming waliingia mtaani mnamo Mei 4, 2013 kupinga mpango wa kuzalisha kemikali zenye sumu karibu na makazi yao. Vyombo vya Habari vya serikali havikutangaza habari za maandamano hayo, na katika hali ya kushangaza wafuatiliaji wa mtandaoni wamefuta habari na picha zinazohusiana na maandamano hayo kwenye mtandao maarufu wa kijamii uitwao Sina Weibo tangu Mei 4, 2013.