Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Februari, 2014
Mchora Katuni wa Algeria Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 18 Jela kwa Kumdhihaki Rais
Djamel Ghanem anakabiliwa na kifungo cha jela kwa kuchora katuni inayoufananisha mpango wa Rais wa Aljeria Abdelaziz Bouteflika wa awamu ya nne na nepi ya mtoto. Katuni hiyo, hata hivyo haikuwahi kuchapishwa
Mbinu za Uvuvi Endelevu kwa Wavuvi wa Dhivehi
Mwanablogu wa MaldiviHani Amir anaandika kuhusu mbinu za uvuvi asilia ikiwa ni pamoja na kukamata mamia ya samaki kwa mikono yao, badala ya kutumia nyavu au fimbo. Mwanablogu huyo pia anatoa mwangaza kuhusu namna wanavyonnyonywa na wamiliki walafi wa hoteli wnaojaribu kuwaibia kwa kutokuwalipa kile wanachostahili.
Madagaska Bado Inasubiri Waziri Mkuu, Serikali Mpya
Mwezi mzima tangu Rais mteule Hery Rajaonarimampianina achaguliwe kuwa mkuu wa nchi nchini Madagaska, bado hakuna dalili nani atakuwa waziri mkuu na akina nani wataunda serikali. Ma-Laza anahoji kuwa suala kuu si hasa nani atakuwa waziri mkuu bali atakuwa ana ajenda gani akikabidhiwa ofisi [fr]: Un technicien hors pair, rassembleur,...