· Juni, 2013

Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Juni, 2013

Kufilisika kwa Watu nchini Malaysia

  30 Juni 2013

iMoney.my wametengeneza mchoro unaoelezea takwimu za kufilisika nchini Malaysia. Wastani wa matukio 20,000 ya kufilisika yamerekodiwa mwaka 2012 hiyo na maana kwamba wa-Malaysia 53 wanafilisika kila siku.

Athari za Mazingira kwa Uchimbaji Madini Nchini Indonesia

  13 Juni 2013

Makala iliyochapishwa katika mtandao wa mongabay.com imefichua athari za uharibifu wa kimazingira ziazotokana na shughuli za uchimbaji madini katika maeneo ya vijiji nchini Indonesia. Baadhi ya wanazuoni wanahofia kwamba maeneo mengi nchini Indonesia yana kiwango cha juu kabisa cha zebaki duniani.

Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?

Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa kufanya manunuzi miongoni mwa watumishi wa umma. Mengineyo ni uwezekano wa kupata fursa ya elimu, huduma ya maji safi, huduma...