· Julai, 2010

Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Julai, 2010

Niger: Njaa ya Kimya Kimya

Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005.

Thailand: Vurugu Zinazotokana na Ujumbe Mfupi wa Maneno wa Waziri Mkuu

  27 Julai 2010

Wakati Waziri mkuu wa Thailand Abhisit Vejjajiva alipotwaa madaraka mwaka 2008, alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mamilioni ya wateja wa simu za viganjani wa Thailand akiwataka wawe na umoja. Hivi sasa anakabiliwa na makosa ya ufisadi kwa kupokea "zawadi" kutoka mashirika ya mawasiliano. Kadhalika anashutumiwa kwa kuvunja mipaka ya ya faragha za wateja wa simu za viganjani.

China: Nchi Imara, Watu Maskini

  9 Julai 2010

Shirika la utangazaji la taifa CCTV liliweka wazi mnamo tarehe 28 Juni kuwa China inatarajia kupata yuani trilioni 8 (sawa na dola trilioni 1.18) katika mapato ya fedha kufikia mwisho wa 2010. Mapato hayo kitaifanya China kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa mapato ya fedha baada ya Marekani. Inaoneka...