Habari kuhusu Majanga kutoka Aprili, 2014
Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini
Zimetimu siku 14 tangu kivuko cha Sewol kizame na watu 205 wamethibitika kupoteza maisha. Wanasiasa wanatumia tukio hilo na habari zisizosahihi za vyombo vya habari kuchochea hasira miongoni mwa Wakorea Kusini.
Kupotea kwa Ndege ya MH370: Waziri Mkuu wa Australia Ajichanganya
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott anazungumza kuhusu zoezi la utafutaji wa ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH370.
Watu 28 Wafariki, 268 Bado Hawajulikani Walipo Baada ya Feri ya Korea Kusini Kuzama
Feri ya Korea Kusini iliyokuwa ikielekea kwenye kisiwa cha mapumziko ilizama ikiwa na mamia ya abiria. Mwongoza mferi hiyo na wafanyakazi wa feri hiyo waliokolewa kwanza, kabla ya abiria wengi kupata msaada
Chanzo cha Maji nchini China Chawekwa Kemikali Inayosababisha Kansa
Benzene, kemikali inayosababisha kansa kwa haraka kabisa, imegundulika kuwepo kwenye chanzo cha maji cha Jiji la Lanzhou , wakati fulani ilipimwa na kukutwa kwa kiwango cha mara 20 zaidi ya kile kinachofahamika kuwa ni salama kwa matumizi.
Tetemeko la Ardhi la Ukubwa wa 6.2 Latokea Nchini Nicaragua
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ukubwa wa 6.1 lilitokea Nicaragua mnamo Alhamisi Aprili 10, 2014. Kulikuwa na taarifa [es] za watu kujeruhiwa na kuanguka kwa nyumba shauri ya mtikisiko mkubwa. Kitovu kilikuwa kilomita 20 Kaskazini ya mji mkuu Managua, karibu na volkano ya Apoyeque, wa kina cha kilomita 10. Katika...
Tetemeko Kubwa Lizitikisa Chile na Peru
Watumiaji wa mtandao wa twita wameripoti kuwa huduma za simu za mkononi hazipatikani na umeme umekatika kwenye maeneo kadhaa ya Peru.
Tetemeko Kubwa Laitikisa Chile Kaskazini, Lafuatiwa na Tahadhari ya Tsunami
Tetemeko kubwa lenye vipimo vya 8.2 limeikumba Chile kaskazini saa 2:46 na kusababisha tahadhari ya tsunami nchini kote.