Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanabeba ‘mzigo maradufu’ kutokana na mashambulizi ya mtandaoni pamoja na udhalilishaji
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanaubeba mzigo maradufu wa dhuluma inayotokana na jinsia mtandaoni ikiwa ni pamoja na vitisho vinavyohusiana na kuripoti taarifa za kisiasa. Vitisho hivi vinavyoendelea vimesababisha waandishi wa habari wanawake kujiondoa kwenye nyuga za umma.
Kukifanya Kiswahili kionekane: Utambulisho, lugha na Mtandao
Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa sana, lakini muonekano wake mtandaoni ni finyu zaidi. Mwanaharakati wa lugha kutoka Kenya Bonface Witaba anapambana kubadili hali hii.
#MatrikiUtambulisho: Mazungumzo ya Twita yanayoangazia utambulisho na haki za kidijitali barani Africa
Wanaharakati kutoka Burkina Faso, Nijeria, Afrika Kusini na Kenya, wataongoza mazungumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia lugha zao za asili kuhusu masuala ya lugha, makabila na haki za kidijitali barani Afrika.
Mwandishi wa Habari Tanzania Atekwa na Kufunguliwa Mashtaka Yenye Utata
Mwandishi Erick Kabendera ameandika kukoa ukandamizaji unaoendelea kuotoa mizizi chini ya Rais wa Tanzania John Magufuli. Jana, serikali ilimhukumu kwa makosa ya kiuchumi, lakini wakosoaji wanasema 'jinai kubwa aliyoifanya ni kuwa mwandishi wa habari.
Kukamatwa kwa Mwandishi Mchunguzi Ivan Golunov Kwaleta Mageuzi katika Jamii ya Urusi
Kukamatwa kwa Golunov kumechochea kuungwa mkono kutoka pande zote za maeneo ya kisiasa nchini Urusi.
Benin Yashuhudia Kuzimwa kwa Mtandao Siku ya Uchaguzi
Mtandao kufungwa ambapo ulifunguliwa usiku, ukiwaacha wapiga kura gizani siku ya uchaguzi.
Wanaharakati Nchini Colombia Wawasilisha Barua Kuhusu Mauaji ya Viongozi wa Kijamii Huko ICC
Zaidi ya viongozi 163 wa kijamii na wanaharakati wameuawa kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita nchini Colombia.
Mtunga Sheria wa Kike wa Brazili Ashambuliwa Mitandaoni Kwa Kuvaa Nguo Zinazoonesha Maumbile
"Ushiriki wa wanawake wenye jamii ni mdogo kiasi kwamba suala la mavazi linaweza kukuzwa kupindukia."
Mwanaharakati Ahmed Mansoor Aliyefungwa UAE Aendelea na Mgomo wa Kutokula
Mansoor anatumikia miaka kumi jela baada ya mahakama kumhukumu kwa kuchapisha habari za uongo na umbea kwenye mitandao ya kijamii.
Wanawake Wanaongoza Maandamano Nchini Sudan
“Wanawake wako mbele, kushoto, na katikati mwa mapinduzi. Maandamano yalipoanza, watu walidai, "Wanawake wangebaki nyumbani.' Lakini sisi tulisema — hapana.”