· Novemba, 2013

Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Novemba, 2013

Kufuatilia Kongamano la Dunia la Demokrasia 2013

  29 Novemba 2013

Kongamano la Dunia la Demokrasia kwa sasa linafanyika mjini Strasbourg, Ufaransa kwa mara ya ppili tangu lianze. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “kuunganisha Taasisi na Wananchi katika Kizazi hiki cha dijitali”. Fuatilia mada nne na warsha 21 za mkutano kupitia alama ashiria #CoE_WFD. 

Sera ya Taarifa ya Uwazi Yahitaji Kuboreshwa zaidi Nchini Japan

  22 Novemba 2013

Pamoja na kuwa serikali ya Japan inajitahidi kupiga hatua katika uboreshaji wa sera yake ya uwazi, nchi hii bado ina safari ndefu, kwani imeshika nafasi ya 30 kati ya nchi 70, kwa mujibu wa orodha liyoandaliwa na Asasi ya Ujuzi Huru. Masahiko Shoji wa Asasi ya Ujuzi Huru nchini Japani aandika:...

Udadisi wa Sami Anan

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.

“Nchi” Nzuri ya Afrika

Katika toleo la wikii hii la Brainstorm, jarida la mtandaoni la Kikenya, Brenda Wambui hulaani masimulizi ya sasa kuhusu Afrika: “Afrika ni nchi”, “Afrika inapaa”, ‘”Mitindo ya Kiafrika.” Huchunguza jinsi Wakenya wanavyoweza kukomboa simulizi lao na kujiainisha kwa kuweka masharti yao wenyewe: Kama wenyeji wa Kenya ama nchi nyingine ile,...

Wahamiaji 87 Wafariki kwa Kukosa Maji Kaskazini mwa Niger

Mnamo tarehe 30 0ctoba, watu 87 waliokuwa wakijaribu kuifikia bahari ya Mediterania walifariki mara baada ya madereva waliokuwa wakiendesha magari waliyoyatumia kusafiria kuwatelekeza wahamiaji hao katika Jangwa la Sahara. Wahamiaji hawa walihangaika kutafuta msaada bila ya mafanikio. Simulizi ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa watu walionusurika aliyejulikana kwa jina la...