· Aprili, 2013

Habari kuhusu Harakati za Mtandaoni kutoka Aprili, 2013

Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi

RuNet Echo  30 Aprili 2013

Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa.

Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.

  28 Aprili 2013

Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.

Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka

RuNet Echo  15 Aprili 2013

Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika manne yaliyolengwa ni wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Voronezh [ru]: ni Vuguvugu la Haki za Binadmau linaloendeshwa na...