Sauti za Iran ni mradi ulioundwa kwa kutumia mafanikio ya mradi wa Ushahidi. Sauti za Iran inakusudia kuripoti habari kuhusu miji midogo na vijiji vya Iran na vile vile kukusanya maombi na matatizo ya wananchi na kuyatuma kwa serikali na wabunge.
Habari Maalum Kuhusu Digital Activism
Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi

Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa.
-
Hakuna Usalama kwa Waandishi wa Kiraia Nchini Bahrain
1 Januari 2013
-
Waandamanaji wa Hangari Wafunga Daraja, Wanafunzi Watatu Watiwa Nguvuni.
1 Januari 2013
-
Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa
31 Disemba 2012
-
Kupigia Kura Maajabu Saba ya Dunia barani Afrika
27 Disemba 2012
-
Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru
28 Agosti 2012
Habari mpya Kuhusu Digital Activism
6 Mei 2013

TEDXSão Tomé: Mkutano Wanukia São Tomé na Príncipe

TEDXSão Tomé
Uandikishaji wa awali kwa ajili ya mkutano wa TEDXSão Tomé umezinduliwa rasmi. Mkutano huo una kaulimbiu inayosema “Visiwa Vimeunganishwa : São Tomé + Príncipe = Áfrika Vimeunganishwa na Ulimwengu” na utafanyika tarehe 20 Juni. Wasemaji katika mkutano huo waliothibitishwa ni pamoja: Dynka Amorim, Ismael Sequeira, Profesa Robert Drewes na Aoaní d'Alva. Tiketi linapatikana kwa Euro 20. Zaidi kuhusu mkutano huo tembelea ukurasa wa Facebook na tovuti [viungo vyote katika lugha ya Kireno].
15 Aprili 2013
Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka

Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika...
27 Februari 2013
Bulgaria: Gharama Kubwa za Nishati Zasababisha Maandamano
Ruslan Trad anataarifu kuwa, siku ya Jumapili tarehe 17 Februari, makumi ya maelfu ya watu katika mji mkuu wa Bulgaria, Sofia pamoja na majiji mengine waliendelea na maandamano kupinga bei kubwa za nishati ya umeme pamoja na gharama za kupasha joto.
29 Januari 2013

Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko
Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.
22 Januari 2013

“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali

Mazungumzo ya kila siku kwa njia ya skype(kwa Kifaransa) kati ya Awa Traoré aliyeko Bamako na Anne Morin akiwa Ufaransa (kupitia anuani ya @annagueye)
Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.
2 Januari 2013

Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan
Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano wa watu.
Israel Yoroba jijini Abidjan anaripoti kuhusu msongamano huo wa kutisha [fr] wakati watu wengi wakiwa wamekusanyika kusubiri kushuhudia milipuko ya fataki kuashirika mwaka mpya katika wilaya ya Plateau. Alama habari #drameplateau ilianzishwa kutoa nafasi ya kupatikana kwa habari za wakati huo huo kuhusu tukio hilo la kusikitisha na namna ya kuwasaidia waathirika. Hili nijanga la tatu la namna hii tangu mwaka 2009 [fr] nchini Côte d'Ivoire.
1 Januari 2013

Kuhusiana na Vuguvugu la Mabadiliko ya Umma
Gaurav Mishra anachambua nguvu ya vuguvugu la mabadiliko linaloanzia kwa watu wa kawaida na namna inavyofanya kazi kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa vyombo vikuu vya habari kwa kutumia vyombo vya habari vya kiraia.
22 Novemba 2012

Dunia Iwatetee Wanablogu Raia wa Vietnam Waliofungwa Gerezani

Nguyen Hoang Vi, Mwanablogu raia wa Vietnam aliyetupwa gerezani kwa sababu ya kuandika maoni yaliyoikosoa serikali
16 Oktoba 2012

Madagascar: Global Voices katika Kimalagasi Yapiga Hatua Kubwa
Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya ki-Malagasi umechapisha mtandaoni posti yake ya 5,000. Mradi huo ulianza mwezi Septemba 12, 2007 ukiwa kati ya miradi ya mwanzo kabisa ya Mradi mkubwa wa Lugha za Kiafrika. Kwa sasa mradi huo unaendeshwa na watafsiri wa ki-Malagasi wapatao 16 miongoni mwao akiwamo mmoja wa watafsiri wadogo kabisa wa Global Voices , mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Radifera Felana Candy.




























Kiungo cha RSS kwa Digital Activism 














Interesting and made me think