The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Diaspora Hifadhi ya mada

Kiungo cha RSS kwa Diaspora

2009-11-16

Sub-Saharan Africa ,
Americas

Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii kutoka Martinique [Fr].

2009-10-24

East Asia

Raia wa kigeni ambaye alitumia muda wa miezi saba iliyopita katika jela ya Beijing No. 1 Detention Center aliitumia idhaa ya DANWEI maelezo ya kina ya maisha yake ya kila siku katika jela hiyo.

2009-02-27

Sudani: Maombolezo ya Mwandishi Maarufu wa Riwaya na Mahakama ya Kimataifa

Baada ya kimya kirefu, wanablogu wa Kisudani, wamerejea kwenye ulimwengu wa blogu kuongea, na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya hivi karibuni. Mawazo hayo yanayojumuishwa katika muhtasari huu ni pamoja na yale ya wanablogu tuliowazoea. Baada ya malalamiko kuhusu hali mbaya ya usalama wa afya kwenye Uwanja wa Ndege wa Khartoum, Msudani mwenye matumaini anaomboleza kifo cha mwandishi wa riwaya mashuhuri, Al- Tayeb Saleh.

2009-02-22

Paraguai: Wahamiaji Wasimulia Visa Vyao

Ni jambo la kawaida katika Marekani ya Latini kwa wahamiaji kuondoka na kwenda kwenye malisho ya kijani zaidi kwenye nchi jirani au nchi za mbali. Hakuna tofauti kwa Waparaguai, ambao huwaacha nyuma marafiki zao na familia ili kufuata fursa nyingine. Simulizi kadhaa za namna hiyo zinasimuliwa kwenye blogu inayoitwa Paraguayos (sisi ni Waparaguai), ambayo inawaalika wahamiaji walioko duniani kote kuwasilisha simulizi zinazohusu uzoefu wao.

2009-01-11

Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele

Mdahalo unaodadisi ni kwa nini vita katika Mashariki ya Kongo vinapewa kipaumbele kidogo ikilinganishwa na migogoro inayotokea Mashariki ya kati. Mwandishi wa habari wa Rue89 anauliza, "ikiwa kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?" Wanablogu wa pande zote mbili wanalichambua swala hilo.

2008-10-21

Madagascar: Kuishi ughaibuni hubadili uhusiano

Katika makala iliyochapishwa mwezi Machi, wachumi William Easterly na Yaw Nyarko wanaeleza kwamba katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara, kiasi cha fedha kinachotumwa na wahamiaji wanaotoka bara hilo ni wastani wa asilimia 81 ya misaada ya fedha kutoka nchi za kigeni kwa kila nchi. Dhima ya waMadagascar walio nchi ...

2008-08-31

Angola, Brazil: Mshituko na Utengano wa KitamaduniPhotos post

Mahusiano maalum kati ya Angola na Brazili yanamaanisha kwamba biashara kati ya makoloni haya mawili ya zamani ya Ureno inashamiri - kadhalika uhamiaji kutoka pande zote za Atlantiki. Lakini, ni vipi hawa watoto wawili wanavyoishi? Ujumbe huu unatoa mitazamo ya wote, kutoka kwa bloga wa Kiangola na wa Kibrazili waishio Luanda.

2008-08-20

Karibeani: Radi ya Bolt Yaipiga Beijing

Olympics
“Radi ya Bolt” - Picha na hybridvigour. Tembelea mtiririko wa picha zake. Ujumbe huu utakuwa mrefu kama ufupi wa mtoko wa Mjamaika Usain Bolt kuelekea chaki ya ukomo wa mbio za mita 100 na utukufu wa Olimpiki ulivyokuwa mfupi na mtamu - kwa sababu mabloga wa Karibiani bado hawajashuka kutoka kilele ...