· Januari, 2010

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Januari, 2010

Rais wa Malawi kutangaza rasmi penzi lake siku ya Valentine

Wamalawi wanatafakari taarifa kuwa mnamo tarehe 1 Mei, rais wa nchi Dkt. Bingu wa Mutharika anatarajiwa kumuoa waziri wa zamani wa utalii Callister Moyo. Harusi hiyo itatanguliwa na sherehe za kitamaduni za uchumba wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino tarehe 14 Februari. Wanabloga wachache wamemtakia heri rais katika mapenzi mapya aliyoyapata baada ya kifo cha mkewe Ethel miaka mitatu iliyopita.

Misri: wanablogu Watiwa Mbaroni Kufuatia Kutembelea kwao Naha Hammady

Leo Misri iliwatia mbaroni wanablogu 20 waliokuwa wakitembelea eneo la Naga Hammady huko Misri ya Juu ili kutoa heshima zao kwa watu waliouwawa katika shambulio la kidini mnano January 7 mwaka huu. Watu 7 waliuwawa kwa risasi huku wengine wengi wakijeruhiwa pale mwuaji alipowamiminia risasi Wakristo wa Madhehebu ya Kikopti waliokuwa wakitoka kanisani mara baada ya Misa ya Krismas (Wakopti husherehekea Krismas kila tarehe 7 Januari). Uamuzi wa kutembelea eneo hilo uliofanywa na wanablogu hao ulikuwa ni kwa lengo la kuungana dhidi ya uhasama wa kidini.

Haiti: Uenezaji Habari na Taarifa

  17 Januari 2010

Sisi tulio nje ya Haiti tunaweza tu kujenga picha kichwani kuhusu hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo huko baada ya tetemeko baya la ardhi - lakini katikati ya juhudi za kuwatafuta wapendwa ndugu, juhudi za kuwahudumia waliojeruhiwa na jukumu zito na gumu la kuwafikishia msaada wa kiutu wale wanaouhitaji zaidi - wanablogu walio huko Port-au-Prince na maeneo ya jirani wanawasiliana na ulimwengu wa nje, ambao nao unahangaika kutaka kupata taarifa kutoka kwa wale waliokuwa katika eneo lenyewe kabisa la janga.

Haiti: Twita Kutoka Eneo La Tukio

  17 Januari 2010

Wakati habari za tetemeko la ardhi huko Haiti zikitoa mwangwi duniani kote, wakazi majasiri, wanahabari wan je, na wafanyakazi wa misaada wanaandika jumbe za twita kutokea katika eneo lililoathirika. Baadhi yao wanafanya kazi ya kukusanya misaada na fedha, wakati wengine wanajaribu tu kuionyesha dunia mambo yanavyooendelea nchini Haiti.

Slovakia, Hungaria: Heri ya Mwaka Mpya!

  6 Januari 2010

Uhusiano kati ya nchi mbili jirani za Slovakia na Hungaria ulianza kutetereka katika mwaka uliopita - lakini baadhi ya wananchi wa Slovakia na Hungaria wanafanya juhudi kurekebisha hali hiyo kwa kuzindua kampeni ya mtandaoni inayojulikana kama "Štastný nový rok, Slovensko! / Boldog Új Évet Magyarország!" ("Heri ya Mwaka Mpya, Slovakia!/Heri ya Mwaka Mpya, Hungaria!).

Kuchapisha Bloguni kuhusu Utamaduni na Ndoa za Watu wa Asili Tofauti

  6 Januari 2010

Idadi kadhaa ya familia zinazoundwa na watu wa rangi na dini tofauti wanasimulia kuhusu uzoefu wa maisha yao katika familia zao kupitia ulimwengu wa blogu. Majaribu na mahangaiko ya wanandoa wenye asili tofauti yanaonyesha, kama kioo, jinsi sisi, kama watu tuliostaarabika, tulivyotoka mbali na hasa katika kupokea na kuheshimu tofauti zetu.