Habari maalum kuhusu Business
Papa Nchini Kameruni (1): Utata wa Safisha-safisha Jijini Yaounde
Papa Benedikti wa XVI anazuru Kameruni kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 20 Machi 2009. Ziara hii imepelekea serikali kuchukua hatua kali za usafi, ambazo zimezua utata mkubwa katika ulimwengu wa blogu nchini Kameruni.
2009-11-06
2009-11-04
Misri: Watu 10 Wenye Ushawishi Zaidi Nchini
Mtoto wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak, anayitwa Gamal Mubarak, -- na ambaye anatarajiwa kumrithi baba yake nafasi hiyo -- aliibuka kama mmoja wa washindi 100 wa TIME. Wanablogu wa Ki-Misri wana ya kueleza kuhusu jambo hili.
2009-02-02
Mashariki ya Kati: Vikwazo kama Silaha ya Kisiasa
Watu wengi wa Mashariki ya Kati wamesusia bidhaa za Israeli na Marekani kama jibu la mashambulizi ya Israeli huko Gaza. Tarek Amr anapitia yale wanablogu wanayosema kuhusu suala hili.
2008-10-01
Mwangwi wa Sakata la Maziwa China katika Afrika
Nchini China inakadiriwa kuwa watoto 13,000 wameugua tangu sakata la maziwa yasiyofaa kuibuka. Ushawishi na nguvu za China vimeongezeka Afrika, kama ulivyoongezeka uagizwaji wa bidhaa za kila namna, kuanzia viatu vya mazoezi mpaka chakula aina ya tambi. Mabloga hata wale walio mbali kama Kongo au Senegal, wanaguswa na usalama wa bidhaa za kutoka China katika nchi zao, na wanafuatilias habari hiyo (ya maziwa yasiyofaa).
2008-09-14
Colombia: Watu Wanaswa na Mitego ya Upatu
Kwa kupitia picha za video na mtandao wa marafiki wa Facebook, raia wa Colombia, Diego Alejandro, anaweka wazi udanganyifu na utapeli mkubwa uliojificha nyuma ya michezo ya upatu ambayo inatangazwa kama njia mbadala za uwekezaji. Katika nchi ambapo akaunti za benki zimepoteza maana kwa sababu ada za uendeshaji ziko juu kuliko riba anayopata mwenye akaunti, michezo hii ya upatu inayoshawishi kumjaza mtu mapesa, ambapo raia wanalipa kiasi fulani cha pesa ili kujiunga na kisha kuingiza marafiki zao 7 kabla wao hawajaanza kufurahia riba ya juu ajabu (kati ya asilimia 40 mpaka 70) basi imekuwa ni kivutio kikubwa mno.
2008-08-31
Angola, Brazil: Mshituko na Utengano wa Kitamaduni
Mahusiano maalum kati ya Angola na Brazili yanamaanisha kwamba biashara kati ya makoloni haya mawili ya zamani ya Ureno inashamiri - kadhalika uhamiaji kutoka pande zote za Atlantiki. Lakini, ni vipi hawa watoto wawili wanavyoishi? Ujumbe huu unatoa mitazamo ya wote, kutoka kwa bloga wa Kiangola na wa Kibrazili waishio Luanda.
2008-08-08
Msumbiji: 2038?
Msumbiji itakuwaje katika miaka 30 ijayo? Mwana sosiolojia Carlos Serra [pt] anatoa mitizamamo tisa ya falme zilizokufa za Kirumi yaani (Byzantine) na anawakaribisha wasomaji wake kurekebisha mitizamo hivyo kwa kadri ya wanavyoona ni sawa:
1. Lugha ya kireno itakuwa ni mabaki, itazidiwa na lugha ya kiingereza, itakayokuwa ikitumika kiufasaha ...




