· Julai, 2013

Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Julai, 2013

India: Chakula Chenye Sumu Chaua Watoto 24

  18 Julai 2013

Chakula kilichoua wanafunnzi na kuwaacha wengine katika hali mbaya kinasadikiwa kuwa kilichanganyikana na dawa ya kuulia wadudu. Tukio hili linaibua maswali kuhusiana na ubora wa chakula cha mchana wanachopewa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini.

Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."

Obama Barani Afrika: Vita ya Kibiashara na China?

Rais Obama ametembelea bara la Afrika kwa ziara iliyokuwa imepangwa kati ya tarehe 26 mpaka Julai 3, 2013. Hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini baada ya kutembelea Senegali na baadae aliitembelea Tanzania. Wachambuzi wengi wanaoiona safari hiyo kama mpango wa kushindana , kama jaribio la Marekani kupambana na mafanikio ya kiuchumi ya China katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.