· Aprili, 2013

Habari kuhusu Habari za Hivi Punde kutoka Aprili, 2013

Jaribio la Mapinduzi katika Visiwa vya Comoro

  24 Aprili 2013

Jeshi la Pilisi nchini Comoro limesema linawashikilia watu wanaosemekana kuwa wahaini raia wa Kongo na Chadi kwa tuhuma za jaribio la kuiangusha serikali lililofanyika mwisho wa wiki. Linfo.re anaongeza kwamba [fr]: Makamanda wa Jeshi hawakutaka kupambana waziwazi na wahaini hao. Waliamini kwamba ” Kujeruhi raia wa Comoro kwa lengo la...

Misri: Mubarak ahukumiwa kifungo cha maisha

Dunia ilishuhudia wakati mahakama ya Misri  ilipomhukumu aliyekuwa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak na Waziri wake wa Mambo ya Ndani Habib Al Adly kifungo cha maisha hivi leo kufuatia kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji.  Hukumu hiyo ilifikiwa baada ya vikao 49,  masaa 250, na kuandikwa katika kurasa 60,000.

Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo

Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake wakati vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake taswira ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.