GlobalVoices katika

Arts & Culture

Hifadhi ya mada · 52 jumbe


Habari mpya Kuhusu Arts & Culture

7 Mei 2013

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

The Team Tanzania (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia:

[...] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika umri wa utu uzima, vijana hao wanatafuta kujitambua huku wakikabiliwa na misongo mingi ya kifamilia na kiutamaduni.

Michoro ya Dar: Sanaa kwa Maendeleo Endelevu

Dar Sketches (Michoro ya Dar) ni sehemu ya mradi unaoanzia ngazi ya Mtaa jijini Dar Es Salaam, Tanzania ulioanzishwa na msanii na mchoraji Sarah Markes:

Ni katika kuenzi urithi wa kitamaduni na wa sanaa ya ubunifu wa majengo kwa jiji la Dar Es Salaam sambamba na juhudi za kukuza uelewa kwa wananchi juu ua tishio la urithi huu linalotokana na kasi kubwa ya kupanuka holela kwa jiji hilo.

26 Disemba 2012

Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama

Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko] ukweli kwamba kosa lilikuwa ni kile alichokichagua mwanaume ndicho kilichosababisha kushindikana kwa zoezi hilo la kuwakutanisha wenzi.

27 Agosti 2012

Mfumo wa Kipekee wa Kuwapa watoto Majina wa Nchini Myanmar (Burma).

Soma makala hii.

Raia wengi wa Myanmar hawana majina ya ukoo. Je, umewahi kujiuliza wanajaza vipi fomu zinazowadai kujaza majina yao ya mwanzo na ya ukoo, au hata kujiuliza kuwa 'Daw' ina maana gani katika jina la Daw Aung San Suu Kyi? Hapa tutatazama mtindo wa pekee kabisa wa Mynmar wa kutoa majina.

31 Julai 2012

Afrika: Usanii wa Kisasa wa ki-Afrika Mtandaoni

Usanii Afrika blogu inayoonyesha usanii wa kisasa wa ki-Afrika: Usanii Afrika ni blogu iliyozaliwa kutokana na upenzi. Akiwa amezaliwa na kipaji cha ubunifu yeye mwenyewe, mwanablogu, Kirsty Macdonald amekuwa na mahusiano ya karibu na masuala ya sanaa na kujieleza”

23 Juni 2012

Pakistani: Buriani Mehdi Hassan; Mfano wa kuigwa wa Ghazal.

Soma makala hii.

Mehdi Hassan Khan ambaye maarufu alijulikana kama ‘Mfalme wa Ghazal’alifariki dunia Jumatano tarehe 13, Juni, 2012 baada ya kuugua kwa muda mrefu, katika hospitali jijini Karachi nchini Pakistan. wananchi wa Mtandaoni wanattoa salamu zao za mwisho.

India: Kipindi cha Runinga cha Aamir Khan Chaweka Wazi Masuala ya Kijamii

Soma makala hii.

Kipindi kipya cha maongezi kwenye televisheni nchi India kinachoitwa Satyamev Jayate (Ni Ukweli tu Utakaoshinda) kinachoendeshwa na muigizaji na mtengeneza filamu wa Bollywood, Aamir Khan kinaleta na kujadili miiko na masuala moto moto ya kijamii ambayo yanawanasa na kuwavutia WaHaindi wengi zaidi na zaidi. Wananchi wa kwenye mtandao wanatoa maoni yao.

7 Juni 2012

Kitabu kipya cha michezo ya watoto kutoka nchi mbalimbali

Blogu changamfu la Kimataifa, PocketCultures limechapisha limechapisha kitabu kuhusu michezo kumi na tano ya watoto kutoka nchi mbalimbali na amabayo inaweza kuchezwa kwa urahisi na msomaji. Kitabu kinaitwa ‘Games for Kids of the World’ na kinaweza kupatikana kwa bure kwenye iPad, Mac au kwenye kompyuta.

Marekani: Kumbukumbu la Walters Art lachapisha Mkusanyiko wa Picha

Jumba la Kumbukumbu la The Walters Art lililoko Baltimore, Maryland limechapisha zaidi ya picha elfu kumi na tisa kwenye mkusanyiko wa Wikimedia Commons na kuziweka chini ya leseni Creative-Commons. Jumba lenyewe lina mkusanyiko wa michoro kutoka Roma na Ulaya.

31 Mei 2012

Zambia: Maoni na Hisia Tofauti baada ya Mwakilishi Kutolewa kwenye Mashindano ya Big Brother

Soma makala hii.

Kuondolewa kwa mwakilishi wa Zambia, mwanamuziki anayefahamika zaidi kwa jina la Mampi, kutoka katika mashindano yanayoendelea ya Big Brother Africa, kumepokelewa kwa hisia na maoni tofauti miongoni mwa watumiaji wa mtandao. Big Brother Africa: StarGame ni toleo la saba la mfululizo wa mashindano hayo maarufu zaidi barani Afrika yanayoonyesha moja kwa moja kupitia televisheni maisha ya washiriki.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha