Habari kutoka Mtandao wa Teknolojia na Uwazi kutoka Machi, 2010
Siku ya Ada Lovelace: Kuwapongeza Wanawake Wanajishughulisha Kupigania Teknolojia na Uwazi Ulimwenguni
Katika kusherehekea Siku ya Ada Lovelace tunawaletea makala fupifupi kuhusu wanawake kadhaa walio sehemu mbalimbali duniani ambao hutumia teknolojia ili kuzifanya serikali ziwe wazi na zinazowajibika zaidi.
Sudani: Je, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Itafanya Kazi?
Jarida la The Financial Times liliripoti hivi karibuni kuwa mpango wa mamilioni ya dola wa Benki ya Dunia wa kusambaza kompyuta na upatikanaji wa Intaneti huko Juba, mji mkuu wa Sudani ya Kusini, umeshindwa. habari hizi zinazua swali: kelele zinazoambatana na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) zina uhalali?