Habari kutoka RuNet Echo
Wa-Belarusi Waamua Kuchapa Kazi Wakiwa Uchi (Kutii Wito wa Rais)
Watumiaji wa mtandao nchini Belarusi wamekuwa wakivua nguo wakiwa makazini, baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Lukashenka.
Kilichotokea Mbwa ‘Mjamzito’ Alipozikwa Hai huko Voronezh
Serikali ya mtaa iliposhindwa kujibu ombi la msaada, watu kadhaa waliamua kujichukulia hatua, kuondoa matofali na kuchimba kumwokoa mbwa huyo aliyekuwa amebanwa.
Hivi Ndivyo Chechen Inavyokabiliana na Kundi la ISIS
Video ya Kadyrov ikiwaonesha wanaume wa Chechen waliokamatwa kwa kushawishi watu kupitia mitandao ya kijamii ili wajiunge na kundi la ISIS, na wazee wanaoonekana wakiwakaripia ni ndugu zao pamoja na viongozi wa eneo wanaloishi wanaume hao
Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17
Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” Teknolojia ya...
Televisheni ya Taifa Urusi Yahariri Wikipedia Kuibebesha Ukraine Lawama kwa Kuanguka MH17
Mtu mmoja wa televisheni ya Taifa Urus, VGTRK, amehariri makala ya kamusi elezo ya Wikipedia kuhusu kuanguka kwa ndege ya Malaysia MH17 ili kuibebesha Kyiv lawama.
Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine
Wakati kukiwa na hisia zinazozidi kuongezeka kufuatia kuanguka kwa ndege nchi Ukraine, matamshi kadhaa yaliyotolewa na watu maarufu Moscow na Donetsk yamevuta hisia za watu
Namna 10 Ambazo Warusi na Wa-Ukraine Walivyopokea Hotuba ya Putin Kuichukua Crimea
Vyovote mtu anavyojisikia kuhusu suala la Crimea, hotuba [ya Putin], ilikuwa ya kihistoria, na ndiyo ambayo wanablogu waliipokea kwa gumzo, kama ilivyo kawaida yao mtandaoni.
Je, Mwigizaji Maarufu Urusi Amempinga Vladimir Putin?
Nchini Urusi, ni nadra sana kwa yeyote anayeonekana mara kwa mara kwenye televisheni kumkosoa , achilia mbali kumpinga Vladimir Putin. Lakini je, Khabensky alithubutu?
Maandishi ya Facebook Kukosoa Kuivamia Crimea Yamgharimu Mwandishi Ajira
Warusi wanauliza ikiwa Putin anaweza kwenda "kuwavamia" na wao, kama hiyo inamaanisha kuongeza mafungu ya fedha kwa ajili ya majimbo yaliyosahaliwa
Aliyoyaandika Waziri Mkuu wa Urusi Medvedev Kwenye Mtandao wa Facebook Kuhusu Ukraine
Waziri Mkuu wa Urusi Medvedev amechagua eneo lisilotarajiwa kusemea tamko lake kuhusu Yanukovich na namna anavyoiona hali ya uongozi wa kisiasa iliyopo Ukraine.