Bomu lililipuka katika kiwanja cha ndege cha Domodedovo mjini Moscow, kwa uchache vifo vya kadri ya watu kumi vimeripotiwa. Mmiminiko wa Twita unapatikana hapa (RUS) na hapa (RUS, ENG). @ann_mint, ambaye anafanya kazi Domodedovo, alikuwa ni mmoja wa watumiaji wa kwanza wa Twita kuripoti juu ya mlipuko huo; “Kuna wahanga #domodedovo tuombeeni,” aliandika (ENG) dakika chache zilizopita.
Habari mpya kutoka RuNet Echo
30 Aprili 2013
Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi
Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa.
15 Aprili 2013
Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka
Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika...
12 Februari 2013
Wakati Papa Anajiuzulu, Warusi Wajiuzulu kwa Putin
Pasipokutaka kujua matokeo ya kujiuzulu kwa Papa Benedict na athari yake kwa imani ya Kikatoliki au tafsiri ya hatua hiyo kufuatia kashfa ya udhalilishaji iliyowakabili kwa watawa, RuNet walioweka habari hiyo kwenye safu za vichekesho.
25 Januari 2011
17 Oktoba 2010
Urusi: Wanablogu wakutana na Balozi wa Irani, waepa kuhoji masuala nyeti
Mkutano kati ya wanablogu wanaoongoza nchini Urusi na Balozi wa Irani jijini Moscow, siku tatu tu baada ya mwanablogu Hossein Derakshan kuhukumiwa kifungo cha miaka 19.5 jela kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kufanya propaganda zinazoipinga serikali" ulizionyesha wazi juhudi zisizoeleweka za diplomasia ya mtandaoni ya Irani nchini Urusi. Vilevile ulionyesha jinsi maslahi binafsi ya kibiashara pamoja na mtizamo taharuki uliopita kiasi wa baadhi ya wanablogu maarufu wa Urusi.
11 Aprili 2010
Kirigistani: Mapinduzi “Yaliyowekwa kwenye Kumbukumbu”
Mnamo tarehe 6 April, nchi ya Kirigistani ilikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala ambayo hatimaye yaliing'oa serikali pamoja na kusababisha vifo vya watu wengi. Pamoja na kwamba intaneti haikushika usukani katika kuhamasisha maandamano hayo, imetumika sana katika kuhifadhi kumbukumbu za kina za maandamano hayo.
9 Aprili 2010
Urusi: Habari za Mwanzo za Milipuko ya Mabomu
Utaratibu wa Jumatatu asubuhi mjini Moscow ulivunjwa leo na milipuko ya mabomu mawili mabomu ya kujiua, ambayo yaliua watu wapatao 38 na kujeruhi kwa uchache watu wapatao 70. Alexey Sidorenko anatafsiri baadhi ya taarifa za mwanzo kutoka katika ulimwengu blogu za Urusi.
13 Februari 2010
Urusi: Maandamano ya Kupinga Serikali Yaripotiwa na Wanablogu, Yasusiwa na Vyombo Vikuu vya Habari
Wakati maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali nchini Urusi katika muongo uliopita yanazidi kudharauliwa na vyombo vikuu vya habari nchini humo, ulimwengu wa blogu unachemka na makala kadhaa juu ya maandamano hayo na athari zinazoweza kutokea.
20 Disemba 2009
Urusi: Simulizi Tatu za Umaskini Uliokithiri
Mwandishi wa habari mpiga picha wa Urusi, Oleg Klimov, anatusimulia visa vitatu vya umaskini uliokithiri ambavyo alipata kusikia habari zake wakati akisubiri treni katika kituo cha treni cha Syzran, jiji lililo katika eneo la Samara la Urusi.





























Kiungo cha RSS kwa RuNet Echo 







mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...