Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya ki-Malagasi umechapisha mtandaoni posti yake ya 5,000. Mradi huo ulianza mwezi Septemba 12, 2007 ukiwa kati ya miradi ya mwanzo kabisa ya Mradi mkubwa wa Lugha za Kiafrika. Kwa sasa mradi huo unaendeshwa na watafsiri wa ki-Malagasi wapatao 16 miongoni mwao akiwamo mmoja wa watafsiri wadogo kabisa wa Global Voices , mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Radifera Felana Candy.
Habari mpya Kuhusu Blogger Profiles
4 Aprili 2011
Wanablogu wa Kenya Waunda Umoja; BAKE
Mnamo tarehe 25 Machi, wanablogu kadhaa wa Kenya walifanya mkutano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, mkutano uliitishwa na BAKE (Bloggers Association KEnya). Huo ulikuwa mkutano wa 4 uliotokana na msukumo wa wanablogu wakongwe wa Kenya.
29 Disemba 2009
Podikasti: Mahojiano na Sudanese Drima
Sudanese Drima ni jina la bandia la mwandishi wa Kisudani wa Global Voices anayeishi nchini Malaysia. Katika mahojiano haya ya dakika kumi tunajadili jinsi uanahabari wa kijamii unavyoathiri Uislamu, mgogoro wa dafur, na masuala ya nafsi ya Uafrika-Uarabu katika Asia ya Kusini Mashariki.
20 Disemba 2009
Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu
Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.
23 Novemba 2009
Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video
Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli....
6 Novemba 2009
Kutambulisha Sauti Zinazotishwa
Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.
26 Januari 2009
Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009
Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?




























Kiungo cha RSS kwa Blogger Profiles 







mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...