Habari maalum kuhusu Blogger News
Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video

Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli. Wanaharakati hawa wa mtandaoni watatumikia vifungo vya miaka miwili na mwingine miaka miwili na nusu gerezani baada ya mashitaka ...
Kutambulisha Sauti Zinazotishwa
Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.
2009-01-26
Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009
Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?



