· Novemba, 2009

Habari kuhusu Matangazo kutoka Novemba, 2009

Kutambulisha Sauti Zinazotishwa

  6 Novemba 2009

Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.