Habari maalum kuhusu Announcements
Kutambulisha Sauti Zinazotishwa
Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.
Gumzo la moja kwa moja kuhusu Virusi vya ukimwi na Ukimwi mtandaoni Tarehe 6 machi
Mradi wa Rising Voices na Global Voices wanaandaa gumzo la moja kwa moja mtandaoni kwa wanablogu na wanaharakati siku ya Ijumaa mwezi wa tatu mwaka huu(saa 11 jioni kwa saa za Nairobi) mada kuu ikiwa jinsi ya kublogu na kuongeza uelewa na habari kuhusu virusi vya ukimwi na Ukimwi.



