Habari maalum kuhusu Swahili
Afrika: Ujio wa Mkonga wa Seacom Wazua Mjadala
Ujio wa mkonga unaopita chini ya bahari utakao ongeza uwezo na kupunguza gharama za intaneti barani Afrika umewasha majadiliano na mvuto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika. Seacom, ambayo inaunganisha Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji na Ulaya pamoja na Asia, ilianza kutumika moja kwa moja Alhamisi, kwa kuziunganisha nchi za Afrika ya mashariki na Afrika ya kusini kwenye mtandao wa dunia wenye wigo mpana.
Pakistani: Musharraf Aondoka Jengoni
Imepita miaka nane, siku mia tatu na ushee tangu mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu yaliyoongozwa na Jenerali wa Jeshi la Pakistani yalipofanyika na hivyo kumpokonya madaraka kiongozi fisadi Nawaz Sharif. Wakati huo kulikuwa na matumaini ya kesho mpya, ilikuwa ni mwendo wa madaha kuelekea kwenye dira iliyofifia iliyopachikwa jina la ...
2008-09-06
Saudi Arabia: Kina Mama Huru
WAKATI kukiwa hakuna shaka kwamba kuna vizuizi kwa wanawake waishio Saudi Arabia, havifanani na taswira iliyojengwa na wageni dhidi ya taifa hilo. Katika makala hii tunao ushauri kwa wakina mama wanaotaka kutembelea jiji la Jeddah wakiwa peke yao, kuna muhtasari wa hoteli za kina mama pekee jijini Riyadh, na wito kwa wageni wote wanajihisi kuzungumza kwa niana ya kina mama wanaokandamizwa wa Saudia.



