The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Spanish Hifadhi ya lugha Katika Makundi

Kiungo cha RSS kwa Spanish

2009-02-22

Paraguai: Wahamiaji Wasimulia Visa Vyao

Ni jambo la kawaida katika Marekani ya Latini kwa wahamiaji kuondoka na kwenda kwenye malisho ya kijani zaidi kwenye nchi jirani au nchi za mbali. Hakuna tofauti kwa Waparaguai, ambao huwaacha nyuma marafiki zao na familia ili kufuata fursa nyingine. Simulizi kadhaa za namna hiyo zinasimuliwa kwenye blogu inayoitwa Paraguayos (sisi ni Waparaguai), ambayo inawaalika wahamiaji walioko duniani kote kuwasilisha simulizi zinazohusu uzoefu wao.

2009-01-28

Meksiko: Mtaalamu wa Kuzuia Utekaji Nyara Atekwa

Meksiko inakabiliwa na wimbi la uhalifu wa jinai, ambamo wote raia wa ndani na wageni wanaviziwa kutekwa nyara. Tukio la karibuni lilitokea katika Saltillo, Coahuila, wakati mtaalamu wa kuzuia utekaji nyara wa Marekani, Felix Batista alitekwa na watu waliovaa vinyafo usoni. Batista alikuwapo nchini humo kuendesha semina kama mfanyakazi wa ...

2008-10-28

Chile: Mkutano wa McCain na Pinochet Mwaka 1985

Mwaka 1985, Mbunge wa bunge la Marekani aitwaye John Mccain alizuru nchini Chile na kukutana na mtawala wa kiimla Augusto Pinochet, akiwa na viongozi wengine wa serikali. Mkutano huo ambao haujawahi kuripotiwa hapo awali umewekwa wazi na mwandishi wa habari John Dinges, ambaye amechapisha habari hiyo kwenye blogu yake CIPHER [es], kadhalika katika blogu ya Huffington Post, ambako huwa anaandika masuala yanayomhusu John McCain "ambaye amekuwa akishutumu vikali dhana ya kuketi na watawala wa kiimla bila ya masharti yoyote, inaonekana kuwa alifanya jambo hilo hilo analolipinga.

2008-10-14

Marekani ya Kusini:Taarifa,Twita kwa Waandishi wa Habari Yapata Umaarufu

"Reporting On" ni zana mpya ya kublogu kwa kifupi na inachukua umaarufu mkubwa katika kundi la wanahabari wa Marekani ya Kusini (Walatino) ambao wanatumia zana hii ili kupashana habari na wengine kuhusu yale wanayoyaandika.

2008-09-14

Colombia: Watu Wanaswa na Mitego ya UpatuVideo post

Kwa kupitia picha za video na mtandao wa marafiki wa Facebook, raia wa Colombia, Diego Alejandro, anaweka wazi udanganyifu na utapeli mkubwa uliojificha nyuma ya michezo ya upatu ambayo inatangazwa kama njia mbadala za uwekezaji. Katika nchi ambapo akaunti za benki zimepoteza maana kwa sababu ada za uendeshaji ziko juu kuliko riba anayopata mwenye akaunti, michezo hii ya upatu inayoshawishi kumjaza mtu mapesa, ambapo raia wanalipa kiasi fulani cha pesa ili kujiunga na kisha kuingiza marafiki zao 7 kabla wao hawajaanza kufurahia riba ya juu ajabu (kati ya asilimia 40 mpaka 70) basi imekuwa ni kivutio kikubwa mno.

2008-09-12

Paraguai: Rais Lugo Kutopokea Mshahara

Utawala wa Rais Ferdinand Lugo umeanza na tangazo kuwa hatapokea mshahara wake wa mwezi. "Sihitaji mshahara huo, ambao unapaswa kumilikiwa na masikini," alisema Lugo. Mabloga nchini humo wanatofautiana mitazamo, wakati mmoja anausifu uamuzi huo, mwingine anajiuliza ni vipi Rais lugo atajilipia gharama binafsi za maisha.

Paraguai: Kuapishwa Kwa Lugo Kwenye Flickr

Rais wa paraguai alianza kutumia Flickr mnamo januari 2008 kama njia ya kuorodhesha nyendo zake wakati wa kampeni. Baada ya kuapishwa kama rais wa nchi siku ya tarehe 15 Agosti, anaendelea kutumia chombo hiki cha uandishi wa kijamii. Karibia picha 2,500 baadaye na zote chini ya haki miliki huria, Lugo anategemea kuwajumuisha WaParaguai nyumbani na ughaibuni katika urais wake.

2008-09-06

Venezuela: Wahindi wa Yukpa, Chavez na Mgogoro wa ArdhiVideo post

Picha za video zinazotumwa kwenye mtandao wa internet na vyombo vya habari vya kiraia zinaonyesha yale yanayojiri kuhusu mgogoro unaoibuka nchini Venezuela kati ya Wahindi wa jamii ya Yukpa wanaoishi katika milima ya Perijá, wamiliki wa ardhi na Rais Chávez. Mgogoro huu kuhusu mipaka ya ardhi umekuwapo kwa takribani miaka 30, yaani tangu pale vikosi vya jeshi vilipowandoa kwa nguvu wanajamii wenyeji ya Ki-Yukpa na kuwapa ardhi hiyo wamiliki wapya walioanzisha mashamba makubwa ya mifugo, hasa ng'ombe, ambao wameendelea kuitumia ardhi hiyo tangu wakati huo.