Habari kuhusu Kihispania kutoka Aprili, 2015
VIDEO: Dunia Inasema #WanabloguZone9WaachiweHuru
Global Voices inakumbuka mwaka mmoja tangu kuwekwa kizuizini kwa wanablogu wa Ethiopia wa Zone9 kwa kutengeneza video hii ya kuwaunga mkono. Sema pamoja nasi: #WanabloguZone9WaachiweHuru!
‘Kulea Mtoto Ukiwa Mtoto': Idadi Kubwa ya Mimba za Utotoni Nchini Venezuela
Desireé Lozano, anayeblogu kwenye blogu ya Voces Visibles, anatoa mwito kwa ongezeko kubwa la mimba za utotoni nchini Venezuela, ambapo asilimia 25 ya mimba ni za vijana, na kukosekana kwa sera sahihi za kudhibiti tatizo hili na matokeo yake. Takwimu za Venezuela zinaonesha kwamba nchi hiyo ina idadi kubwa ya...
Je, Blogu Zinaelekea Kutoweka?
Makala haya ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (#JumatatuYaBloguGlobalVoices) siku ya Machi 23, 2015. Kwenye #LunesDeBlogsGV (#JumatatuyaBloguGlobalVoices), tunajitahidi kuzitunza blogu mithili ya “viumbe wanaoelekea kutoweka”, kwa kushughulikia changamto zinazokabili uwepo wa blogu kwenye ulimwengu wa kidijitali. Jitihada kama hizi zinamfanya mwanablogu Iván Lasso kuchambua mustakabali wa kublogu na matatizo yanayowakabili wanablogu leo,...
Kulinda Taarifa Binafsi Nchini Ajentina Bado Kuna Safari Ndefu
Kwenye makala iliyoandikwa kwa ajili ya gazeti la mtandaoni Haki za Kidijitali: Amerika Kusini & Visiwa vya Caribbean, No.21, Mmwanasheria wa ki-Ajentina Valeria Milanés anaeleza kwamba hata kama Marekani ni kiranja wa dunia kwenye kuchakata taarifa (data), bado haina sheria ya kulinda taarifa za watu. Marekani pia inachukuliwa kama nchi yenye “kiwango...
Nini Tofauti ya Kusoma na Kuelimika?
Pedro Muller anatafakari kuhusu matatizo yanayoukabili mfumo wa shule, taasisi anayosema ilimaanisha mazingira tofauti ya kihistoria. Kwa kusema hayo, anabainisha umuhimu wa dhana hizi mbili zinazofanana lakini zikimaanisha nyakati mbili tofauti: “Kusoma” na “kuelimika”: El educar se va más allá de memorizarse un par de nombres y olvidarlos al siguiente...
Umoja wa Ulaya Hautatoa Nafuu ya Kodi ya VAT kwa Vitabu ya Kidigitali
Mnamo Machi 5, 2015, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwamba punguzo la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) lililotolewa kwa vitabu vinavyochapishwa halitahusisha vitabu vya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kila kinachosambazwa au kutolewa kwa mfumo wa kieletroniki au kwa mtandao wa intaneti ni huduma. Amalia Lopez anahoji...
Mwizi Akamatwa, Aomba Msamaha na Kusamehewa
Labda alidhani ingekuwa vyepesi kuiba shampoo mali ya mmiliki wa duka nchini Peru, lakini mambo yalimwendea mrama mwizi huyu. Mtu mmoja akiwa ameongozana na mwenzake waliingia kwenye duka lililoko kwenye jiji la Huancayo nchini Peru, wakisema walikuwa wanataka kununua pombe, na mmiliki alipokuwa amepumbazwa kidogo, jamaa walibeba boksi la shampoo....
Kudhibitiwa kwa Sanaa ya Michoro ya Uchi Kuna Maana Gani Kwetu na Mitandao ya Kijamii?
Makala haya ni sehemu ya kwanza ya mfululizo unaoangazia namna tofauti za ufuatiliaji wanazokabiliana nazo wasanii mtandaoni. Msingi wetu utakuwa uzoefu wa msanii wa Venezuela Erika Ordisgotti.