The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

French Hifadhi ya lugha Katika Makundi

Kiungo cha RSS kwa French

2009-02-15

Haiti: Fanmi Lavalas na Uchaguzi Ujao

Mwishoni mwa juma lililopita, ulimwengu wa wanablogu wa Kihaiti ulijaa habari za kutengwa kwa vyama vya siasa na Tume ya Muda ya Uchaguzi kwenye uchaguzi wa maseneta utakaofanyika mwezi Aprili 2009 , na siku ya tarehe 6 Januari, tume hiyo CEP ilichapisha orodha ya wagombea ubunge watakaokwaana kwenye uchaguzi ujao wa bunge nchini Haiti. Wanablogu wanaandika mawazo yao kuhusu wagombea walioachwa.

2009-02-09

Madagaska: Zaidi ya 25 Wauwawa Katika Maandamano Kuelekea Ikulu

Watu wapatao 25 walipigwa risasi na kuuwawa leo katika mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wakati wa maandamano ya kuelekea ikulu ya nchi hiyo yaliyoitishwa na meya wa jiji Andry Rajoelina baada ya kujitangaza kama kiongozi wa serikali mpya ya mpito katika mkutano wa hadhara wa kisiasa. Katika majuma yaliyopita, ugombeaji wa nguvu za kisiasa kati ya Meya na Rais Marc Ravolamanana kumesababisha ghasia na uporaji.

Karibeani Ya Kifaransa: Tamasha la Kanivali 2009 LazinduliwaPhotos post

Kanavali ni utamaduni, sehemu ya uhai wa kila Muhindi wa Magharibi bila kuwaacha wale wa Karibeani ya Kifaransa. Ufuatao ni muhtasari wa blogu kutoka Martiniki, Guyana ya Kifaransa, Haiti na Guadalupe, ambao unaelezea mambo yanavyokuwa kwenye Kanivali.

2009-01-27

Madagaska: Kimbunga Chasababisha Kimbunga Cha KisiasaPhotos post

Baada ya siku chache kupita nchini Madagaska, idadi rasmi ya madhara yaliyosababishwa na kimbunga kilichopewa jina la Fanele zimewasilishwa. Rais Ravalomanana alikwenda kwenye moja ya maeneo yaliathirika na kimbunga ili kutathmini madhara yaliyotokea. Uandishi wa kiraia wakati wa kimbunga Wakati idara inayoangalia athari na majanga, BGNRC bado haina tovuti, taarifa zinahusu ...

2009-01-11

Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele

Mdahalo unaodadisi ni kwa nini vita katika Mashariki ya Kongo vinapewa kipaumbele kidogo ikilinganishwa na migogoro inayotokea Mashariki ya kati. Mwandishi wa habari wa Rue89 anauliza, "ikiwa kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?" Wanablogu wa pande zote mbili wanalichambua swala hilo.

2008-11-02

Kongo: Utata Watawala Goma

Miezi miwili iliyopita mapigano yamezuka tena katika jimbo la mashariki la Kivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya kundi la upinzani linaloongozwa na Jenerali laurtent Nkunda na majeshi ya serikali, kinyume na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi januari. Mapambano hayo yameongezeka zaidi katika siku 6 zilizopita na, japokuwa usitishaji wa vita hivyo ulitangazwa, hali bado ni ya kutananisha mjini Goma. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa wanablogu walioko sehemu hiyo.

2008-10-01

Mwangwi wa Sakata la Maziwa China katika Afrika

Nchini China inakadiriwa kuwa watoto 13,000 wameugua tangu sakata la maziwa yasiyofaa kuibuka. Ushawishi na nguvu za China vimeongezeka Afrika, kama ulivyoongezeka uagizwaji wa bidhaa za kila namna, kuanzia viatu vya mazoezi mpaka chakula aina ya tambi. Mabloga hata wale walio mbali kama Kongo au Senegal, wanaguswa na usalama wa bidhaa za kutoka China katika nchi zao, na wanafuatilias habari hiyo (ya maziwa yasiyofaa).

2008-08-17

Arabeyes: Rais wa Mauritania Aliyepinduliwa Katika mapinduzi ya Kijeshi

MAKAMANDA wa jeshi wamemuondoa madarakani Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi, rais wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi huru katika miongo miwili, katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatano iliyopita baada ya mtafaruku wa kisiasa uliotokana na rais huyo kuwatimua kazi majenerali wanne wa ngazi za juu wa jeshi. Makamanda wa jeshi ...