The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Farsi Hifadhi ya lugha Katika Makundi

Kiungo cha RSS kwa Farsi

2009-06-16

Irani: Maandamano na UkandamizajiVideo post

Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Husein Mousavi huku wakiipuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.

2009-06-14

Irani: Kimbunga cha Maandamano Baada Ya UchaguziVideo post

Maelfu ya watu waliandamana mjini Tehran, Mashdad na kwenye miji mingine mikubwa ya Irani ili kupinga ushindi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa. Washindani wawili wanamageuzi pamoja na mashabiki wao wanasisitiza kwamba palitokea udanganyifu.

2009-06-13

Ramani ya Ulimwengu wa Blogu za Irani Siku ya Mkesha wa Uchaguzi

John Kelly na Bruce Etling wanaelezea utafiti wao unaohusu ulimwengu wa blogu za Irani na uchaguzi katika blogu ya Intaneti na Demokrasi. Intaneti na Demokrasi ni blogu ya timu ya mradi wa Intaneti na Demokrasi wa Kituo cha Berkman cha Intaneti & Jamii kilichoko Harvard. Kufuatana na ufuatiliaji wetu wa ...

Uchaguzi Wa Irani Katika PichaPhotos post

Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne tu kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao wamepewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea katika uchaguzi. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu walikuwa wakiwapigia debe wagombea wanaowapenda.

2009-04-10

Irani: Mwaka Mpya Waanza na Ujumbe Kutoka Kwa ObamaVideo post

Siku Wairani waliposherehekea Norouz (Nowruz) kama sikukuu ya mwaka mpya nchini Irani, raisi wa Marekani Barak Obama alituma ujumbe kwa watu wa Irani na kwa viongozi wa Jamhuri ya kiislamu, ujumbe huo ulitoa rai ya kutaka mwanzo mpya kati ya nchi hizo mbili. Wanablogu kadhaa wametoa maoni kuhusu ujumbe huo, angalia baadhi ya maoni hayo.

2009-01-11

Serikali Ya Irani Yautumia Mgogoro Wa Gaza Kukandamiza

Wakati wanablogu kadhaa wa Kiirani (pamoja na wale wa-Kiislamu) waliongeza makala zao na jitihada nyingine za kidijitali, kama vile "Google bomb" kulaani uvamizi wa Israeli katika ukanda wa Gaza, wanablogu wengine wanasema kwamba serikali ya Irani inatumia 'mwanya wa mgogoro wa Gaza' kukandamiza vyombo vya habari na jumuiya za kiraia ndani ya nchi hiyo.

2008-09-21

Irani: Redio Zamaneh, Redio ya Mabloga

Redio Zamaneh ni redio ya lugha ya kipersia yenye makao yake huko mjini Amsterdam. Zamaneh ni neno linalomaanisha "wakati" katika lugha hiyo. Redio Zamaneh (RZ) ni chombo huru cha utangazaji kilichosajiliwa kama asasi isiyo ya kiserikali huko Uholanzi, kikiwa na studio na makao yake makuu mjini Amsterdam. Mratibu wa ...

2008-08-31

Waziri matatani kwa cheti ‘feki'

Ali Kordan,Waziri wa Mambo ya Ndani wa Irani, Katika siku za hivi karibuni, ameshutumiwa vikali kwa kuonyesha Shahada 'feki' ya Udaktari (PhD) aliyodai kupata kutoka katika chuo kikuu chenye sifa kubwa duniani cha Oxford cha nchini Uingereza. Tovuti mbalimbali, pamoja na ile ya kihafidhina wa Alef, zimechapisha ...