Habari kuhusu Kiingereza kutoka Mei, 2015
Baada ya Miaka 33, Cuba Haipo Kwenye Orodha ya Marekani ya Nchi Zinazofadhili Ugaidi
Orodha hiyo, kwa mujibu wa Marekani, ni ya nchi ambazo zina kawaida ya kuwezesha vitendo vya ngazi ya kimataifa vilivyopangwa, na vyenye lengo la kupambana kisiasa na raia wasio na silaha.
ISIS Yashambulikia Kwa Mara Nyingine Msikiti wa Shia Nchini Saudi Arabia
kwenye dawati lakuthibitisha habari la Global Voices, mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Meedan Checkdesk, zana ya mtandaoni ya kufuatilia habari, na Global Voices Online, Joey Ayoub anaonesha miitikio ya awali kabisa kuhusu kupigwa bomu kwa msikiti wa pili wa Shia huko Dammam, Jimbo la Mashariki mwa Saudi Arabia, siku...
Vito na Sarafu za Kale za Syria Zapigwa Mnada Kwenye Mtandao wa Facebook
Sarafu za kale zilizoibwa na ISIS kutoka kwenye maeneo yanayodhibitiwa na ISIS, sasa yanapigwa mnada kwenye mtandao na Facebook kwa mamilioni.
Je, Saudi Arabia Imelishambulia Bwawa la Kale la Marib Nchini Yemen?
Kuna taarifa zisizodhibitishwa zinazosema kwamba vikosi vya pamoja vya Kisaudi, ambavyo vimekuwa vikiishambulia Yemen kwa mabomu kwa zaidi ya miezi miwili sasa vimelilenga Bwawa la Marib, moja wapo ya maajabu makuu ya katika ulimwengu wa ubunifu wa kale wa kiufundi. Kwenye mtandao wa Twita, Hussain Albukhaiti anadai: Unconfirmed reports: #Saudi...
Uchaguzi wa FIFA Unaendelea
Pamoja na kutiwa nguvuni kwa maafisa kadhaa wa FIFA kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Wizara ya Sheria ya Marekani, chombo hicho kinachosimamia kandanda duniani kimesema kwamba uchaguzi wake, ambao utaunda baraza la 65 la FIFA, utaendelea kama ulivyopangwa hivi leo. Rais wa FIFA aliye madarakani Sepp Blatter, ambaye ameongoza chombo hicho...
Lugha za Pili Zinazoongozwa Kuzungumzwa Zaidi Afrika
Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo: Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.”...
Mwanablogu wa Ethiopia, Atnaf Berahane: Kijana Anayejiamini, Aliye Gerezani
Ndoto ya uhuru wa kujieleza ya mwanablogu huyu mwenye umri wa miaka 26 imemplelekea kupokonywa uhuru wake.
Tunayoyajua na Tusiyoyajua Baada ya Jaribio la Mapinduzi Nchini Burundi
Celebration and jubilation near Presidential offices in Bujumbura after the overthrow of Nkurunziza. #BurundiCoup pic.twitter.com/WhJzXKfS69 — Robert ALAI (@RobertAlai) May 13, 2015 Shangwe na vifijo karibu na ikulu ya Rais nchini Bujumbura baada ya kupinduliwa kwa Nkurunzisa. Kufuatia nia ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu ya Rais wa Burundi...