Habari kuhusu Kiingereza kutoka Aprili, 2015
VIDEO: Dunia Inasema #WanabloguZone9WaachiweHuru
Global Voices inakumbuka mwaka mmoja tangu kuwekwa kizuizini kwa wanablogu wa Ethiopia wa Zone9 kwa kutengeneza video hii ya kuwaunga mkono. Sema pamoja nasi: #WanabloguZone9WaachiweHuru!
Swali: Wapiganaji Wangapi wa Jihadi Wana Historia ya Jeshi?
Kwa kutumia dondoo kutoka kwenye ripoti ya Der Spiegel kuhusu watu walionyuma ya muundo wa ISIS, mwanablogu wa Palestina Iyad El-Baghdadi anatwiti: After that Spiegel story about the "mastermind" behind ISIS's takeover of Syria – noticed just how many Jihadists have military backgrounds? — Iyad El-Baghdadi (@iyad_elbaghdadi) April 21, 2015...
Maisha ya Wakenya Yana Thamani, Wanafunzi wa Kiafrika Wasema Kwenye Ibada ya Kuwaombea Wahanga wa Garissa Jijini Beijing
Kikundi cha wanafunzi wa Kiafrika jijini Beijing waliandaa ibada ya kuwakumbuka wahanga 147 wa shambulio la Garissa pamoja na china kutokuwa na uvumilivu kwa watu wanaoomboleza hadharani
Filamu ya Malawi Yawasaidia Wakulima Kujikinga na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Filamu ya “Mbeu Yosintha” ilitengenezwa kuwasaidia wakulima na wanavijiji kujikinga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, hususani kubadilika kwa majira ya mvua kwenye ukanda wa Afrika Kusini Mashariki. Filamu hiyo ni tamthlia inayowatumia wasanii wa ndani ya nchi hiyo na iliandaliwa na mwandishi wa Kimalawi Jonathan Mbuna baada ya...
Misri Yamhukumu Rais wa Zamani Morsi Miaka 20 Jela kwa “Utishaji na Matumizi ya Nguvu” Dhidi ya Waandamanaji
Misri imemhukumu rais wake wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi kifungo cha miaka 20 jela leo, bada ya kukuta na hatia ya "utishaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi" kwa waandamanaji mwaka 2012.
GVFace: Kuvunja Ukimya wa Pakistani Kuhusu Mapigano Yanayoendelea Jimbo la Balochistani
Mijadala wa wazi kuhusu vita vinavyoendelea kwenye jimbo la Balochistani ni nadra. Wanaotetea umoja wa nchi hiyo wanadhani kimya kuhusu jimbo Balochistan ni wajibu wao wa kizalendo, wengine wakijizuia kwa hofu ya nguvu ya kijeshi ya Pakistani.
Mchora Katuni wa Malaysia Aapa Kuendelea Kupambana na Serikali Licha ya Kushitakiwa kwa Uchochezi
"Sitanyamaza. Ninawezaje kutokuwa na upande, wakati hata penseli yangu ina upande!"
Muswada wa Uhalifu wa Mtandaoni Unawapa Mamlaka Zaidi Polisi, Kuliko Wananchi
Wapinzani wakuu wa muswada huo kutoka kwenye asasi za kiraia wanasema wataipeleka serikali mahakamani kama rais ataidhinisha muswada huo kuwa sheria.
Afrika Kusini Imejitenga na Waafrika Wengine?
Mashambulizi ya hivi karibuni huko Afrika Kusini yanahusisha wahamiaji kupigwa, kuuawa, kuchomwa moto, wizi madukani pamoja na wizi wa mali zao. Watu watano wameshauawa, miongoni mwao akiwamo mvulana wa miaka 14 aliyeuawa siku ya jumatatu.
Je, Waganda Wameridhika na Utendaji wa Serikali Yao Kama Matokeo ya Utafiti Yanavyoonesha?
"Historia inatuambia kwamba watu HAWAKUI ili kuupenda na kuuenzi udikteta bali kinyume chake."