Habari kuhusu Kiingereza kutoka Mei, 2014
Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia
Ghasia, zilizofumuka baada ya kuuawa kwa kijana wa miaka 19, zilisababisha misuguano kati ya watu wenye asili ya Albania na Masedonia kwenye jiji la Skopje.
Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti
Kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji wa Kitibeti Gepe nchini China,hapa ni mtiririko wa matukio ya jinsi hiyo sambamba na video za nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube.
Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini
Ingawa Rwanda imepiga hatua kubwa katika kuponya majeraha ya mauaji ya kimbari ya 1994, makundi ya utetezi yanaripoti vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu.
Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu
Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ameshinda urais kwa kishindo, huku akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye ameshika nafasi ya tatu. Baada ya siku tatu za zoezi la upigaji kura, Sisi ameshinda kwa asilimia 93.3 ya kura zote. Hamdeen alipata asilimia 3 wakati asilimia 3.7 zimeharibika.
Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?
Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka: Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa Zambia Michael Chilufya Sata, aliye madarakani tangu Septemba 2011. Tetesi hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba serikali...
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
Naibu Waziri Ajinyonga baada ya Kushindwa Uchaguzi Nchini Malawi
Blogu ya City Press inaandika kwamba kujinyonga kwa Godfrey Kamanya, Naibu Wairi wa Malawi, baada ya kushindwa kukitetea kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, 2014 : Matangazo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne bado yanaendelea kutangazwa. Lakini matokeo ya awali ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na kituo cha redio yalionyesha...
Uchaguzi wa Malawi 2014
Malawi inapiga kura kumchagua rais siku ya Jumanne Mei 20, 2014. Fuatilia taarifa za moja kwa moja kwenye mtandao wa Twita @Malawi2014 na @MEIC_2014.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
“Hatujaweka Mkazo vya Kutosha Kwenye Afya ya Vijana”
Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu afya ya vijana duniani inabainisha kwamba: Sababu kubwa za vifo vya vijana duniani ni ajali za barabarani, VVU?UKIMWI, na kujiua. Duniani kote, wastani wa vijana milioni 1.3 walipoteza maisha yao mwaka 2012. Ripoti inaongeza vile vile kuwa :...