Habari kuhusu Kiingereza kutoka Septemba, 2009
Philippines:Mafuriko Mabaya Zaidi Katika Kipindi cha Miaka 40
Kimbunga kilichopewa jina la 'Ondoy" kimeikumba Philippines jumamosi iliyopita na kusababisha mafuriko mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 40 ambayo yamesababisha vifo vya watu 50 na kusababisha wakazi 280, 000 kupoteza makazi. Tovuti za kijamii zilipashana habari za kimbunga hicho na jinsi ya kuwasaidia walioathirika.
Marekani: Stempu ya Iddi Yachochea Chuki Huko Tennessee
Barua pepe yenye madai ya uongo kuwa Rais Obama ametoa stempu mpya kuadhimisha sikukuu ya Waislamu Eid al-Fitr imemfikia Meya wa Tennessee ambaye aliisambaza kwa wafanyakazi wake na waasa waisusie stempu hiyo.
Uganda: Blogu,Twita Zaipasha Habari Dunia Wakati Machafuko Yanaendelea Mjini Kampala
Wakati machafuko yalipoitingisha Kampala, mji mkuu wa Uganda, kwa siku ya pili, wanablogu na watumiaji wa intaneti waliungana ili kuupasha ulimwengu habari.