· Januari, 2009

Below are posts about citizen media in English. Don't miss Global Voices, where Global Voices posts are translated into English! Read about our Lingua project to learn more about how Global Voices content is being translated into other languages.

Habari kuhusu Kiingereza kutoka Januari, 2009

Meksiko: Mtaalamu wa Kuzuia Utekaji Nyara Atekwa

  28 Januari 2009

Meksiko inakabiliwa na wimbi la uhalifu wa jinai, ambamo wote raia wa ndani na wageni wanaviziwa kutekwa nyara. Tukio la karibuni lilitokea katika Saltillo, Coahuila, wakati mtaalamu wa kuzuia utekaji nyara wa Marekani, Felix Batista alitekwa na watu waliovaa vinyafo usoni. Batista alikuwapo nchini humo kuendesha semina kama mfanyakazi wa...

Madagaska: Kimbunga Chasababisha Kimbunga Cha Kisiasa

  27 Januari 2009

Baada ya siku chache kupita nchini Madagaska, idadi rasmi ya madhara yaliyosababishwa na kimbunga kilichopewa jina la Fanele zimewasilishwa. Rais Ravalomanana alikwenda kwenye moja ya maeneo yaliathirika na kimbunga ili kutathmini madhara yaliyotokea. Uandishi wa kiraia wakati wa kimbunga Wakati idara inayoangalia athari na majanga, BGNRC bado haina tovuti, taarifa...

Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009

  26 Januari 2009

Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?

Malaysia: Mafunzo Yanayotokana na Mafuriko

  21 Januari 2009

Wiki iliyopita, mafuriko yaliyakumba maeneo mbalimbali katika jimbo la Sarawak nchini Malaysia. Wanablogu wanaandika yaliyotukia na mafunzo yaliyotokana na janga hilo la mafuriko. Mafuriko hayo ni mabaya zaidi kutokea katika miaka mingi nchini Malaysia.

Ugiriki: Malalamiko Kuhusu Usafirishwaji wa Silaha kuelekea Israeli

  20 Januari 2009

Wakati vita vikiendelea huko Gaza, taarifa zilizotolewa mwanzoni mwa mwezi kuhusu shehena kubwa ya silaha kutoka Marekani kuelekea Israeli kupitia bandari ya Astakos huko Ugiriki zimezua kelele kutoka kwa wanablogu wa Kigiriki. Wanablogu hao walitumia huduma ya Twita kuchunguza swala hilo na kuitia shinikizo serikali ya Ugiriki kusimamisha usafirishwaji wa silaha hizo.

Palestina: Mawasiliano na Gaza

Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.

Kuhusu habari zetu za Kiingereza

en