Habari kuhusu Kichina kutoka Disemba, 2009
China na Iran: #CN4Iran
Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji wa Ki-China wa twita wanatumia alama ya #cn4iran ili kuonyesha mshikamano na wenzao wa Irani.
China: Kujitoa Uhai kwa Msomi Mwingine tena – Kisa cha Yang Yuanyuan
YANG Yuanyuan, binti msomi mwenye miaka 30 aliyekuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Shanghai Maritime, alijinyonga kwenye bafu la nyumbani kwake mnamo Novemba 25 mwaka huu. Siku moja kabla hajachukua uamuzi huo alimwambia mama yake kwamba maarifa hayawezi kubadili majaaliwa. Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia ongezeko la...
China: Uvunjaji Nyumba kwa Kutumia Mabavu
Visa viwili vya uvunjaji nyumba kwa mabavu vimeibua hisia za kutaka kulindwa zaidi kwa haki za raia na utatuzi wa migogoro nchini Uchina. Watumiaji wa mtandao wa Kichina wanatoa maoni.
China: Barafu Iliyotengezwa Uchina
Jumapili hii iliyopita tarehe 1 Novemba, Beijing ilishuhudia kuanguka kwa mapema zaidi kwa theluji katika miaka 22 iliyopita. Badiliko hilo la ghafla la hali ya hewa, lililofunika kabisa mji mzima kwa barafu, liliwashangaza wakazi wengi. Lakini vyombo vya habari viliripoti baadaye kwamba uangukaji huo wa barafu ulisababishwa na ofisi ya...