The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Arabic Hifadhi ya lugha Katika Makundi

Kiungo cha RSS kwa Arabic

2008-10-26

Misri: Sisi sote ni Laila

Sisi sote ni Laila, ndivyo wanavyosikika kusema kwa sauti moja wanablogu wa kike wa Misri. Hivi, huyu Laila ni nani na kwa nini wasichana na wanawake wa kiMisri wanapenda kufananishwa naye? Hebu endelea kusoma ili uone ni kwa namna gani wanablogu wa Misri wanavyojihangaisha ili kuvunjilia mbali vikwazo vya jinsia na kufanya sauti zao zisikike.

2008-10-15

Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa MarekaniVideo post

Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.

2008-09-12

Jordan: Ubloga wa Video wa Malkia RaniaVideo post

Chombo cha habari cha Blogger Times kinachoendeshwa na mabloga wa Kiarabu, kimemtaja Malkia Rania wa Jordan kuwa bloga maarufu zaidi wa video za kutoka Uarabuni katika chombo cha Video mtandaoni, YouTube, kufuatia mafanikio ya mlolongo wa video za YouTube aliouanzisha kuondoa dhana potofu dhidi ya Waarabu.

2008-08-17

Arabeyes: Rais wa Mauritania Aliyepinduliwa Katika mapinduzi ya Kijeshi

MAKAMANDA wa jeshi wamemuondoa madarakani Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi, rais wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi huru katika miongo miwili, katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatano iliyopita baada ya mtafaruku wa kisiasa uliotokana na rais huyo kuwatimua kazi majenerali wanne wa ngazi za juu wa jeshi. Makamanda wa jeshi ...