Habari kuhusu Kiarabu kutoka Julai, 2014
Israel Yaanza Operesheni ya Ardhini Gaza
Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku kumi za mapigano yaliyogharimu maisha ya wa-Palestina 200. Hatua hiyo inafuatia Hamas kukataa pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Misri.
Nchini Tunisia, Swali ni Ikiwa ni Lazima Kupiga Kura au Kugomea Uchaguzi
Kadri uchaguzi unavyokaribia nchini Tunisia, watumiaji wa mtandao wanajadili ikiwa uchaguzi huo unastahili kupewa heshima ya kura zao ili kuwachagua wabunge na rais
Misri Yapandisha Bei ya Mafuta Hadi Asilimia 78
Wamisri watumiao mtandao wamekasirishwa na ongezeko la bei ya mafuta, hatua ambayo wanasema itasababisha kupanda kwa gharama za usafiri, chakula na hata huduma nyingine za jamii.